Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Papa Francis awarai viongozi wa Sudan Kusini kukomesha machafuko

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, anayeendelea na ziara yake nchini Sudan Kusini, amesema Kanisa haliwezi kusalia kimya na badala yake linapaswa kupaza sauti, kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu na matumizi mabaya ya madaraka.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis akiwa na rais Salva Kiir na viongozi wengine wa Kanisa, wakiwa katika Ikulu ya Juba, Februari 03 2023
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis akiwa na rais Salva Kiir na viongozi wengine wa Kanisa, wakiwa katika Ikulu ya Juba, Februari 03 2023 REUTERS - YARA NARDI
Matangazo ya kibiashara

Papa Francis, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Makasisi na Watawa, katika Kanisa kuu la Mtakatifu Theresa jijini Juba.

Katika ziara hiyo anayoandamana na Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby, kutoka Kanisa Angilikana,  wamelaani kuendelea kwa vita na mauaji ya mara kwa mara nchini humo, na kuwataka viongozi wa kisiasa wa nchi hiyo, rais Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa rais Riek Machar, kuhakiikisha machafuko, ukabila na ufisadi vinakoma.

Aidha, Papa Francis amekutana na waathiriwa wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe jijini Juba, katika taifa hilo ambalo kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, watu zaidi ya Milioni Mbili, wameyakimbia makwao kwa sababu ya vita.

Kiongozi huyo, anayezuru Sudan Kusini kwa mara ya Kwanza, nchi iliyoapata uhuru mwaka 2011, anatarajiwa kutamatisha ziara yake siku ya Jumapili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.