Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: Mapigano yarindima katika maeneo ya Kitshanga na Bwito

Mapigano hayo yameanza tena Jumatano hii, Januari 25 asubuhi kati ya FARDC na M23 kwa upande mmoja na kati ya M23 na Mai-Mai, kwa upande mwingine. Yanatokea kwenye maeneo mawili ya vita katika maeneo ya Masisi na Rutshuru katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC.

Msafara wa magari ya wanajeshi wa FARDC huko Kivu Kaskazini, karibu na Rutshuru.
Msafara wa magari ya wanajeshi wa FARDC huko Kivu Kaskazini, karibu na Rutshuru. AFP PHOTO / Junior D. Kannah
Matangazo ya kibiashara

Mapigano makali yametokea asubuhi katika eneo la Kitshanga, kilomita 2 kutoka mji wa Rugarama. Waasi wa M23 wamejaribu kuuteka mji wa Kitshanga, mji mkubwa wa Masisi, zaidi ya kilomita 80 magharibi mwa Goma, bila mafanikio. Walipata upinzani kutoka kwa jeshi la DRC, vyanzo vya ndani vinaripoti, kulingana na tovuti ya radio OKAPI inayodhaminiwa na Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Lakini walifanikiwa kudhibiti barabara ya Kitshanga-Goma, kutoka Rugarama, kilomita 2 kutoka Kitshanga. Pia wawasi hao wamepiga kambi huko Rushebeshe, kilomita 14 kwenye barabara ya Masisi-Kitshanga.

Hali bado ni ya wasiwasi siku ya Jumatano na vyanzo kadhaa vya habari vinatangaza kusitishwa kwa shughuli kwenye mhimili wa Masisi-Kitshanga tangu asubuhi.

Aidha, baada ya kupunguza msongamano wa magari asubuhi ya leo huko Rushebeshe, mapigano hayo pia yaliripotiwa Monastere, Kabale-Kasha, Burungu na Tebero kuelekea kwenye mashamba.

Sehemu kubwa ya wakazi bado wamezuiliwa mbele ya kituo cha MONUSCO, wakati wengine waliondoka tangu siku ya Jumanne, Januari 24 kwenda Mwesso na kwingineko.

Umuhimu wa Kitshanga

Eneo la Kitshanga ambako mapigano haya yanaripotiwa, ni moja ya maeneo muhimu ya Masisi.

Sio tu kwamba Kitshanga ilikuwa makao makuu ya kundi la kiongozi wa waasi Laurent Nkunda cha National Congress for the Defence of the People (CNDP), lakini pia ni kituo kikuu cha kibiashara cha kijamii na kiuchumi kati ya maeneo kadhaa, kwani inaunganisha barabara ya Goma-Masisi - Walikale.

Kwa kuongeza, mji wa Goma sasa umekatika kutoka kaskazini ya mbali, kwa sababu barabara hii ya Masisi ilibakia kuwa njia pekee ya usambazaji kati ya Goma-Rutshuru-Butembo na Beni.

Magari kadhaa ya abiria yalilazimika kupiga U-turn Jumatano hii kwa pande zote mbili. Hali hii inawatia wasiwasi sana wakazi wa Kivu Kaskazini, ambao wana hatari ya kukosa hewa, kulingana na gavana wa Kivu Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.