Pata taarifa kuu
SIASA-USALAMA

Tundu Lissu kurejea Tanzania tarehe 25 mwezi huu, baada ya kuwa uhamishoni kwa miaa kadhaa

Mwanasiasa wa upinzani, na aliyekuwa mgombea urais nchini Tanzania mwaka 2020, Tundu Lissu, aliyeikimbilia nchini Ubelgiji baada ya kushambuliwa kwa  kupigwa risasi na watu wasiojulikana  mwaka 2017, ametangaza kuwa atarejea nyumbani, tarehe 25 mwezi huu. 

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu. © AFP - stringer
Matangazo ya kibiashara

Lissu ametoa tangazo hilo, siku chache baada ya rais Samia Suluhu Hassan, kutangaza kuondoa marufuku kwa vyama vya upinzani, kuandaa mikutano ya siasa. 

Lissu ameyasema hayo alipokuwa akitoa salamu zake za mwaka 2023 kwa njia ya mtandao akiwa uhamishoni nchini Ubelgiji.

''Muda huo ninatarajia kutua uwanja wa ndege wa kimataifa Dsm kwa Ndege ya Shirika la Ndege Ethiopia nikitokea Brussels Ubelgiji....nitafurahi sana kwa mapokezi yoyote mtakayopendezwa kuniandalia siku hiyo''. Alisema Bw. Lissu.

Nimeishi uhamishoni kwa zaidi ya miaka mitano, kuanzia siku niliyokimbizwa Nairobi Kenya kwa matibabu ya dharura, baada ya jaribio la mauaji dhidi yangu la tarehe 7 Septemba mwaka 2017.

Aidha, rais Samia ameonekana kukumbatia maridhiano ya kisiasa na wanasiasa wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.