DRC: Wanaharakati wana mashaka na ahadi za M23 kuondoka Rumangabo
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, waasi wa M 23 wanatarajiwa kuondoka na kukabidhi Rumangabo, kambi kubwa ya wanajeshi wa DRC kwa vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, baada ya kuahidi kuondoka.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Waharakati wanasema hawaamini iwapo waasi hao wataondoka kabisa katika eneo hilo la kambi ya Rumangambo, baada ya kuondoka kwao mjini Kibumba kutiliwa shaka na jeshi la DRC, kama anavyoeleza HENRI MAHANO, kiongozi wa Shirika la kirai katika eneo hilo.
Wakati hili likitarajiwa, ripoti zinasema jana; waasi hao waliendelea kusonga mbele katika Wilaya ya Rutshuru na kuchukua eneo la Nyamilima.