Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

DRC: Watuhumiwa wa mashambulizi dhidi ya vijiji magharibi mwa DRC wahukumiwa

Watu mia moja wanaotuhumiwa kushiriki katika mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa kati ya mwezi Juni na Novemba magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameanza kusikilizwa na mahakama ya kijeshi ya eneo hilo, chanzo kutoka mahakama kimesema siku ya Alhamisi.

Kijiji cha Kwamouth, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huko Maï-Ndombe.
Kijiji cha Kwamouth, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huko Maï-Ndombe. © Google Maps
Matangazo ya kibiashara

 

Mgogoro huu unahusisha jamii za Teke na Yaka katika maeneo ya Kwamouth (katika mkoa wa Mai-Ndombe) na Bagata (katika mkoa wa Kwilu).

Washtakiwa, wakiwemo askari 28 wa vikosi vya usalama (wanajeshi na maafiosa wa polisi), wanashitakiwa kwa "mauaji, kumiliki silaha kinyume cha sheria, kujiunga na kundi la wahalifu, wizi, kufanya uasi, na mashambulizi", kulingana na 'mashtaka.

Wameshtakiwa tangu Jumanne katika mahakama ya kijeshi ya Bandundu-mjini, katika mkoa wa Kwilu, wakili Prosper Gata, ameliambia shirika la habari la AFP. Watuhumiwa hao ambao wanazuiliwa katika gereza la Cinquantenaire huko Bandundu-mjini, wanakanusha shutma hizo dhidi yao, chanzo hiki kimeongeza.

Kesi inayofuata imepangwa kufanyika Desemba 20. Ghasia zilianza mwezi Juni huko Mai-Ndombe kuhusiana na mzozo wa ardhi na ambao ulienea, hasa katika mkoa jirani wa Kwilu, ambapo mashambulizi dhidi ya vijiji yalisababisha vifo vya watu kadhaa.

Mnamo mwezi Oktoba, serikali ilitangaza idadi ya "zaidi ya watu 180 waliofariki". Mashambulizi hayo mabaya yameendelea tangu wakati huo, hadi kufikia karibu na mji mkuu Kinshasa. Lakini ripoti rasmi ya mashambulizi haya ya hivi punde bado haijachapishwa.

Umoja wa Mataifa umekadiria idadi ya watu waliokimbia makazi yao kuwa makumi kadhaa kwa maelfu, waliofukuzwa kutoka vijiji vyao na mapigano haya kati ya Wateke, ambao wanajiona kuwa wenyeji na wamiliki wa vijiji vilivyoko kando ya Mto Kongo kwa umbali wa kilomita 200 na Waka, waliokuja kuishi katika eneo hilo baada yao.

Baadhi ya watu waliokimbia makazi yao wamevuka mto na kuingia katika nchi jirani ya Congo-Brazzaville, kulingana na vyanzo kutoka mashirika ya kutoa misaada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.