Pata taarifa kuu

Mashirika ya misaada yaonya kutokea kwa janga la kiafya katika kambi za wakimbizi DRC

Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu Mashariki mwa nchi hiyo, wameonya kuwa kuna uwezekano wa kutokea kwa janga la kiafya, kufuatia ongezeko la ugonjwa wa kipindupindu katika kambi za wakimbizi. 

Baadhi ya wananchi walioyakimbia makazi yao katika kambi ya Munigi iliyopo km 5 kutoka mjini Goma.
Baadhi ya wananchi walioyakimbia makazi yao katika kambi ya Munigi iliyopo km 5 kutoka mjini Goma. AFP/Phil Moore
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, linasema kati ya Novemba 26 hadi Desemba tarehe 7, watu 256 wamepata matatibu katika eneo la Munigi karibu na Goma, baada ya kuambukizwa kipindupindu. 

Miongoni mwa watu hao ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano, na kuongeza kuwa, hii ni dalili ya kuongezeka kwa maambukizi hayo. 

Walio kwenye hatari ni maelfu ya watu wanaoishi kwenye kambi wa wakimbizi, hasa Nyiragongo, ambako watu wanaodariwa kuwa zaidi ya Laki Moja na Elfu Sabini, wamekimbilia katika wiki kadhaa zilizopita kwa hofu ya kiusalama. 

Mvua kubwa, inayoedelea kunyesha na ukosefu wa vyuo, ni miongoni mwa sababu zinazoelezwa kusababisha mlipuko wa ugonjwa huo na sasa maisha ya maelfu ya watu, yapo hatarini, na pia kukabiliwa na uhaba wa chakula. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.