Pata taarifa kuu

Mamlaka ya Uganda yafunga shule ili kuzuia kuenea kwa mlipuko wa Ebola

Mwisho wa mwaka wa shule umesogezwa mbele kwa wiki mbili na umepangwa Novemba 25 nchini Uganda, ambapo mlipuko wa virusi vya Ebola tayari umeua watoto wanane tangu Septemba 20, Waziri wa Elimu ametangaza leo Jumanne.

Waziri wa Elimu wa Uganda Janet Museveni, ambaye pia ni mke wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Waziri wa Elimu wa Uganda Janet Museveni, ambaye pia ni mke wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni. ©Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

“Serikali imepitia na kuidhinisha pendekezo la Wizara ya Afya la kupunguza muhula wa tatu kwa wiki mbili ili kupunguza msongamano shuleni jambo ambalo linaweza kuongeza hatari ya watoto kuambukizwa EVD” (ugonjwa wa Ebola), amesema katika taarifa Waziri wa Elimu Janet Museveni, ambaye pia ni mke wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni.

"Shule za kitalu, msingi na sekondari zitafungwa kwa muhula wa tatu siku ya Ijumaa, Novemba 25, 2022," amesema, akiongeza kuwa shule "zitahitajika kuandaa mitihani (...) mapema kidogo kuanzia wiki ijayo."

 

Kufikia sasa ugonjwa wa Ebola umeua watu 53, kati ya kesi 135 za maambukizi, kulingana na takwimu rasmi za tarehe 6 Novemba.

Kulingana na Bi Museveni, visa 23 vya maambukizi vimetambuliwa kwa watoto, wanane kati yao walikufa, na wengine 16 waliwekwa karantini mnamo Novemba 4, 2022 ili kutathmini uwezekano wa kuambukizwa na virusi hivyo.

Watoto 11 wanaosoma shule tano katika mji mkuu wa Kampala, wilaya jirani ya Wakiso na Mubende, ni miongoni mwa watu walioambukizwa, ameongeza.

Kufunga shule mapema kutapunguza maeneo ambayo watoto hukutana kwa karibu na watoto wengine, walimu na wafanyakazi wengine ambao wanaweza kueneza virusi kila siku,” amebain.

Siku ay Jumamosi mamlaka iliongeza kwa wiki tatu kufungwa kwa wilaya mbili katikati mwa nchi, vitovu vya janga hilo, na marufuku ya kusafiri na kufungwa kwa maeneo ya umma.

Ebola mara nyingi ni homa mbaya ya virusi ya hemorrhagic. Ugonjwa huo umepewa jina la mto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambapo uligunduliwa mwaka 1976.

Maambukizi ya binadamu ni kupitia maji maji ya mwili, dalili kuu zikiwa ni homa, kutapika, kutokwa na damu na kuhara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.