Pata taarifa kuu

Yoweri Museveni aomba radhi raia wa Kenya kwa ujumbe wa mwanae kuhusu Kenya

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaomba radhi Wakenya kwa machapisho ya mtoto wake Jenerali Muhoozi Kainerugaba aliyoyatoa, kupitia mtandao wake wa Twitter, akisema jeshi la nchi yake linaweza kuivamia Kenya na kuliteka jiji kuu Nairobi ndani ya wiki mbili.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Januari 16, 2022.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Januari 16, 2022. REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Rais Museveni amesema anajutia kitendo cha mwanaye aliyehamishwa kutoka cheo cha mkuu wa majeshi ya nchi kavu  hadi kuwa jenerali kamili , na ambaye ni mtumishi wa umma alichapisha ujumbe uliongilia maswala ya ndani ya nchi jirani, akisema Kenya ni ndugu wa nchi ya Uganda na marafiki. 

Hata hivyo rais Museveni amesema hatua ya kumpandisha cheo jenerali ni kwa sababu anahisi ana moyo  na uwezo wa kuchangia katika ujenzi wa uzalendo katika ukanda wa Afrika na njia ya kumtia moyo ni kumpa nafasi kujifunza kwa kulaani yaliyo mabaya na kuchochea kilicho jema kwa kuonyesha njia sahihi ya kutumia taasisi za kiukanda kalma umoja wa Afrika na jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Aidha Museveni amesema msamaha  Wake ni kwa pia raia wa Uganda ambao wamechukizwa na matendo ya jenerali Muhoozi. 

Si mara ya kwanza jenerali Muhoozi kuchapisha kwenye mtandao wake wa Twitter, wakati huu akiwakera Wakenya kwa kauli zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.