Pata taarifa kuu

Baada ya mlipuko wa Ebola nchini Uganda, Tanzania yajiandaa

Kwa kukabiliwa na mlipuko mpya wa Ebola nchini Uganda, nchi jirani zinajiandaa kwa kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo. Nchini Tanzania, mamlaka ilitangaza Ijumaa, Septemba 23, kwamba wanamarisha udhibiti wa mipaka yake. Pia imezindua kampeni za uhamasishaji shuleni. Lengo ni kukomesha kuenea kwa homa hii ya hemorrhagic ambayo tayari imeua watu 11 nchini Uganda.

Nyaraka zenye maagizo ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola zilizotolewa na mtaalamu wa afya katika kijiji kimoja magharibi mwa Uganda.
Nyaraka zenye maagizo ya kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola zilizotolewa na mtaalamu wa afya katika kijiji kimoja magharibi mwa Uganda. AP - Ronald Kabuubi
Matangazo ya kibiashara

Tahadhari hiyo imetolewa katika maeneo ya pande zote mbili za Tanzania na Uganda, ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, mji mkuu wa Tanzania, Mwanza na Kagera, kaskazini mwa Kampala. Katika mikoa hii, raia wametakiwa kuwa makini.

“Iwapo watakutana na mtu mwenye dalili za Ebola, lazima watoe tahadhari kwenye kituo cha afya. Kwa kuwa ni ugonjwa wa virusi, dalili zinaweza kuwa homa, kutapika, lakini ishara inayoonekana zaidi ni kutokwa na damu kwenye semu za juu na za siri,  kinywani na puani. Tumeanzisha timu za kukabilian a na hali hiyo ili kubaini maeneo yaliyo hatarini, lazima waende huko na kueleza raia nini wanapaswa kufanya pindi inapotokea maambukizi”, amebainisha Aifello Sichalwe, mkuu wa huduma ya matibabu katika wizara ya Afya ya Tanzania.

Timu za madaktari za watu 12 kwa sasa zinafanya kazi katika mikoa yote 26 ya Tanzania. Ili kupunguza kuenea kwa Ebola, mamlaka ya Tanzania pia imeanzisha vituo vitano vya kuwatenga wagonjwa ili kuwatibu wagonjwa walio na dalili za kwanza, na wanafanya kazi ya kuimarisha ukaguzi kwa wasafiri katika viwanja vya ndege na bandari. Hakuna kesi yaEbola aina ya "Sudan" ambayo imegunduliwa nchini Tanzania.

Mkutano usiokuwa wa kawaida utakaowaleta pamoja madaktari wote wa mikoa utafanyika Jumatatu hii, Septemba 26, ambapo mkakati wa majibu unapaswa kuwa kwenye ajenda ya mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.