Pata taarifa kuu

Bei mpya ya mafuta yatangazwa nchini Kenya

Nchini Kenya, mamlaka ya kudhibiti nishati, imetangaza bei mpya ya mafuta, baada ya rais mpya William Ruto kuapishwa kuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo siku ya Jumanne. 

Wakenya wakiwa kwenye foleni katika kituo cha mafuta cha Nairobi mwaka wa 2018.
Wakenya wakiwa kwenye foleni katika kituo cha mafuta cha Nairobi mwaka wa 2018. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Wakenya wamelalamikia ongezeko hilo ambalo ni la juu katika historia ya bei ya mafuta nchini humo, wakati huu kukiwa na wasiwasi wa kupanda zaidi kwa gharama ya maisha. 

Lita moja ya mafuta ya petroli sasa itauzwa kwa fedha za nchi hiyo, Shilingi 179 ikiwa ni ongezeko la Shilingi 20, na ruzuku iliyokuwa inatolewa na serikali iliyopita, kwa wauza mafuta, imeondolewa. 

Nayo, bei ya mafuta ya dizeli imepanda kwa shilingi 25 na sasa itauzwa kwa Shilingi 165 kwa lita moja, katika jiji kuu la Nairobi. 

Bei ya mafuta nayo, imepanda na sasa itauzwa kwa Shilingi 147. 94. 

Kupanda kwa bei ya mafuta kunatarajiwa kusababisha kupanda kwa gharama ya usafiri na umeme na hivyo kufanya maisha ya wananchi wa kawaida magumu. 

Serikali ya rais Ruto inasema, imeondoa ruzuku ya mafuta kwa sababu, imekuwa haiwasaidii raia wa nchi hiyo wanaoendelea kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.