Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

DRC: Gavana wa Tanganyika aitwa kuelezea usimamizi wake wa ukosefu wa usalama

Nchini DRC, gavana wa mkoa wa Tanganyika ameitwa Alhamisi hii mjini Kinshasa, akiitishwa kwa mashauriano. Julie Ngungwa Mwayuma atajieleza kuhusu usimamizi wa matatizo ya ukosefu wa usalama katika mkoa wake. Katika Wizara ya Mambo ya Ndani, inaelezwa kuwa ni suala la kutoa mwanga kuhusu hali mbaya inayoripotiwa katika mkoa wa Tanganyika. Mbali na ukosefu wa usalama, masuala ya kijamii na kisiasa yatajadiliwa.

Jiji la Kinshasa wakati wa machweo ya jua, Februari 8, 2021.
Jiji la Kinshasa wakati wa machweo ya jua, Februari 8, 2021. © Alexis Huguet, RFI
Matangazo ya kibiashara

Ni wito ambao unapaswa kufanya iwezekane kuangalia hali hii ya usalama katika mkoa wa Tanganyika, ambayo imezorota katika miezi ya hivi karibuni.

wapiganaji wa Mai-Mai, wanaoendesha vitendo vyao viovu bila kuadhibiwa katika eneo la uchimbaji madini huko Mukuyi, eneo la Manono; watoto waliotekwa nyara huko Kalemie, na kupatikana siku chache baadaye katika mkoa wa Kivu Kusini, wakienda kusikojulikana; Wabantu na Watwa wakikabilian hadi kusababisha vifo huko Moba...

Julie Ngungwa Mwayuma analazimika kushughulikia kesi zote hizi, tangu kuapishwa kwake kama gavana baada ya kuchaguliwa kwake Mei mwaka jana.

Pamoja na suala la ukosefu wa usalama, pia atatoa mwanga kuhusu mivutano ya kisiasa na kijamii inayoutikisa mkoa wa Tanganyika. Sehemu ya ofisi ya bunge la mkoa, ambayo shughuli zake zimepigwa marufuku tangu mwishoni mwa mwezi wa Julai, bado linapinga uchaguzi wake, amesema mwangalizi katika eneo hilo. Suala jingine linalozua sintofahamu, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kalemie, walijitokeza barabarani kukashifu ukosefu wa usalama kufuatia mauaji ya mmoja wao.

Gavana pia atatoa maelezo kuhusu mkopo wa dola milioni kumi ambazo aliomba na alipewa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.