Pata taarifa kuu

DRC: Wanajeshi na maafisa polisi waagizwa kuondoka kwenye machimbo ya madini

Uwepo wa askari au maafisa wa polisi hautavumiliwa tena katika machimbo ya madini. Uamuzi wa serikali ya kitaifa ulitokana na unyanyasaji ulioonekana kwenye sehemu hizo na kuwasilishwa Alhamisi hii na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Usalama na Masuala ya Kimila, Jean-Paul Molipo ambaye kwa sasa yuko ziarani huko Grand-Katanga.

Nchini DRC, uchimbaji wa madini huchangia karibu 20% ya uzalishaji wa shaba na kobalti.
Nchini DRC, uchimbaji wa madini huchangia karibu 20% ya uzalishaji wa shaba na kobalti. Β© AFP/John Wessels
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umetokana na uhalifu na vurugu zilizotokea mara kwa mara katika machimbo kadhaa ya madini. Bila kibali kazi, maafisa wa polisi na askari kutoka mikoa mingine ya nchi huvamia maeneo ya migodi na kukaa kwenye machimbo.

Licha ya kuwa na jukumu la kuwasimamia wachimbaji wadogo katika maeneo haya, maafisa wa polisi wenye kusimamia migodi pia wanachangia machafuko haya. Wanarahisishia raia wengi wa kigeni, hasa Wachina, kupitisha mlango wa nyuma madini haya.

Luisha (sio mbali na Lubumbashi), Shikata (nje ya Likasi), Kasolo (katika eneo la Kolwezi), Musebe (katika eneo la Nyunzu) na Luena (huko Haut Lomami) ni baadhi ya maeneo ambayo watu hao waliovalia sare za vikosi vya usalama na ulinzi pia wanafanya shughuli ya uchimbaji wa madini. Raia wanalalamika kuona uzalishaji wake ukinyakuliwa kwa njia hii. Katika ziara hii huko Grand- Katanga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jean-Paul Molipo anatarajia kurejesha utulivu katika sekta hii ya madini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.