Pata taarifa kuu

DRC: Mabaki ya Patrice Lumumba yarejea nchini

Mabaki ya mwili wa Patrice Lumumba yamewasili nchini DRC Jumatano Juni 22, 2022. Kurejea huku kunaashiria kuanza kwa zoezi la siku kumi kote nchini kuonyesha moja ya mabaki ya shujaa huyo wa kitaifa aliyetetea uhuru wa DRC. Fursa hatimaye ya kutoa heshima ya mwisho kwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo aliyeuawa zaidi ya miaka 61 iliyopita.

Ndege iliyobeba mabaki ya mwili wa Patrice Lumumba imetua Kinshasa Jumatano hii, Juni 22, 2022.
Ndege iliyobeba mabaki ya mwili wa Patrice Lumumba imetua Kinshasa Jumatano hii, Juni 22, 2022. © Paulina Zidi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Heshima za kijeshi zilifanyika wakati wa kuondoka kwa mabaki hayo mjini Brussels, heshima za kijeshi zilifanyika wakati ndege iliyobeba mabaki hayo ilipotua katika mji wa DRC, Kinshasa. Asubuhi na mapema, wakati jua lilikuwa limechomoza tu juu ya mji mkuu wa Kongo, ndege iliyobeba mabaki ya Patrice Lumumba, ikiwa na picha ya Waziri Mkuu wa zamani, ilitua katika mji mkuu. Ilikuwa ni wakati mzito kwa wajumbe walioandamana na jeneza na hasa kwa rubani wa ndege aliyepewa heshima ya kusafirisha mabaki ya shujaa wa taifa nyumbani.

Katika ndege iliyoondoka Ubelgiji kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Melsbroek Jumanne jioni, kulikuwa na familia, ujumbe wa serikali ukiongozwa na Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde, wanaharakati na waandishi wa habari. Kwa ujumla, watu mia moja waliohudhuria sherehe zote za kupokea mabaki hayo nchini Ubelgiji.

Hatua hii ya kwanza inaashiria kurejea kwa shujaa wa taifa katika ardhi ya Kongo baada ya miaka 61 ya kusubiri. Baadhi ya wajumbe

 wataandamana na jeneza kuelekea Onalua, kijiji asili cha Patrice Lumumba, huko Sankuru. Jiji lililopewa jina hivi karibuni la "Lumumba-ville".

Msafara huo kisha utaelekea kaskazini, kuelekea Kisangani, ambapo dhamira ya kisiasa ya Patrice Lumumba ilizaliwa kabla ya kuelekea Lubumbashi, huko Katanga. Jeneza la Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo kisha litapelekwa Shilatembo, ambako aliuawa Januari 17, 1961, pamoja na wenzake wawili.

Mabaki ya shujaa wa kitaifa wa DRC yatarejeshwa Kinshasa kwa siku tatu za maombolezo ya kitaifa na sherehe mbele ya viongozi wa kitaifa na kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.