Pata taarifa kuu
UGANDA-DRC-WAASI

Watafiti wasema Uganda ilisukumwa na maslahi ya mafuta kutuma wanajeshi nchini DRC

Watafiti sasa wanasema operesheni za jeshi la Uganda dhidi ya waasi wa  ADF Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa ushirikiano na jeshi la FARDC, ilichochewa zaidia na hatua ya Kampala kutaka kulinda maslahi yake ya mafuta.

Wanajeshi wa Uganda wakiwa Mashariki mwa DRC
Wanajeshi wa Uganda wakiwa Mashariki mwa DRC AFP - PETER BUSOMOKE
Matangazo ya kibiashara

Ripoti iliyotolewa na shirika la utafiti la Congo Research Group (soma hiyo ripoti hapa)  katika chuo kikuu cha New York na Shirika la DRC la utafiti la Ebuteli, inaeleza kuwa baada ya operesheni hiyo kuanza Novemba 2021, kundi la ADF limegawanyika kwa makundi matatu au manne, na limeondoka katika ngome zake.

Maslahi makuu ya Uganda ni kulinda maeneo ya mafuta yanayoamiwa kuwa katika Ziwa Albert, linalopakana na nchi hiyo jirani hali ambayo inaelezwa pia kuipa hofu Rwanda ambayo inaona ushawishi wake Mashariki mwa DRC unafifia.

Watalaam wanaonya kuwa, kujitokeza tena kwa kundi la M 23 sio kwa bahati mbaya, ni jambo ambalo limeonekana kuzuka baada ya operesheni za Uganda, Mashariki mwa DRC.

Licha ya Uganda na DRC kusema kuwa operesheni hiyo imefanikiwa pakubwa kulidhoofisha kundi la ADF ambalo ni la kigaidi, limeendelea kutekeleza mauaji ya raia, Mashariki mwa nchi hiyo.

Aidha, ripoti hiyo haijafanikiwa kuharibu muundo wa ADF, waasi ambao wanaelezwa kuwa na uwezo wa kurejea tena kwenye uwanja wa vita lakini pia linalobadilika kutokana na mazingira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.