Pata taarifa kuu
RWANDA-UINGEREZA

Wahamiaji kutoka nchini Uingereza kuanza kuwasili nchini Rwanda

Kundi la kwanza la wahamiaji 31  kutoka Albania, Iraq, Iran na Syria walioingia nchini Uingereza kinyume cha sheria wanatarajiwa kuwasili nchini Rwanda leo, baada ya Majaji kukataa rufaa ya wanaharakati wa kutetea haki za binadamu waliokuwa wanapinga kusafirishwa kwao.

Wanaharakati wakiandamana  Juni 14, 2022  kupinga mpango wa serikali ya Uingereza kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda
Wanaharakati wakiandamana Juni 14, 2022 kupinga mpango wa serikali ya Uingereza kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda AFP - NIKLAS HALLE'N
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, Mahakama ya rufaa jijini London, ilikataa kesi iliyokuwa imewasilishwa na wanaharakati kutaka serikali ya Uingereza kusitisha mpango wake, hadi pale shauri hilo litakaposikilizwa na uamuzi kutolewa.

“Rufaa hii imekataliwa,” alisema Jaji Rabinder Singh baada ya wiki iliyopita, Mahakama Kuu pia kukataa ombi la wanaharakati wanaosema mpango huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

Mbali na wanaharakati kupinga mpango huu, Tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia wakimbizi UNHCR inasema kinachofanyika hakikubaliki.

 Filippo Grandi ni Mkuu wa UNHCR amesema “Mpango huu ni mbaya, haustahili kutekelezwa, nchi hiyo imesaini mkataba wa kuwalinda wahamiaji, kinachoendelea hakikubaliki, “.

 Mwanamfalme wa Uingereza Charles naye ameonesha masikitiko yake kuhusu mpango huo wa serikali ya Uingereza, ambao amesema unashangaza.

 Mwezi Aprili Uingereza na Rwanda zilitangaza kukubaliana kuhusu mpango huo na sasa mhamiaji haramu atakayeingia katika taifa hilo la bara Ulaya atasafirishwa Kigali.

Rwanda itanufaika kifedha kutokana na mpango huo, huku Uingereza ikisema inapambana na wahamiaji haramu wanaoingia nchini mwake. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.