Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Mauaji yakithiri mashariki mwa DRC, ADF yanyooshewa kidole cha lawama

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watu 11 wameuawa mjini Kokola, Wilayani Beni, hapo jana  baada ya kushambuliwa na waasi wanaoshukia kuwa wa kundi la waasi wa Uganda wa ADF. 

Waasi wa ADF wanyooshewa kidole cha lawama kwa mashambulizi kadhaa, hasa dhidi ya raia. Hapa, wanajeshi wa Kongo wakikagua shambulio karibu na mji wa Oicha, karibu na mji wa Beni.
Waasi wa ADF wanyooshewa kidole cha lawama kwa mashambulizi kadhaa, hasa dhidi ya raia. Hapa, wanajeshi wa Kongo wakikagua shambulio karibu na mji wa Oicha, karibu na mji wa Beni. © Al-hadji Kudra Maliro, AP
Matangazo ya kibiashara

Ni shambulizi ya 7 katika kipindi cha masaa 72 , baadhi ya raia waliojeruhiwa kwa mapanga, walipelekwa hospitalini, kulingana na Gérôme munyambete , msimamizi wa hospitali kuu Mjini OICHA.

Familia nyingi zimeutoroka tena mji huo , ulioanza tena kujijenga baada ya raia wake kurejelea katika makazi  yao, amesema Patric Musubao; kiongozi wa kirai

" Wajaribu kufatilia tena , waongeze Idadi ya wanajeshi , adui hana nguvu kabisa, kwani anakuja bila kujianda kwa vifaa na silaha katika vita, baadayakutekelezauhalifu wake anarudi nyuma. Sisi tunaomba tu serikali iongeze tu idadi ya wanajeshi kama ilivyo kuwa kwa siku zilizopita " 

Jeshi linadai kukomboa mateka 3 waliokuwa wakishikiliwa na waasi hao kulingana na Kanali Charles Omeonga, mkuu kiongozi wa wilaya ya Beni . 

" Ndiyo uwa wanakuja kama wezi , Jeshi ya kwetu ili shughulika nao , ika faulu  , Waka chukua mateka wengine , tuna subiri Sababu Jeshi iko nafatana nao , hali kokola inakuwa shwari , Waasi wali fanya wizi " 

Mwanzoni mwa mwezi huu , raia 16 waliuawa na waasi hao wanao shukiwa kuwa wa ADF mjini Bulongo .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.