Pata taarifa kuu
Sudan Kusini - Usalama

watu 28 wafariki Sudan Kusini katika kisa cha wizi wa mifugo

Watu 28 wameuawa nchini Sudan Kusini katika kisa cha wizi wa mifugo, katika jimbo la Unity.

Mfugaji wa ng'ombe nchini Sudan Kusini
Mfugaji wa ng'ombe nchini Sudan Kusini © AFP - Alex McBride
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa eneo la Leer, Stephen Taker, amesema wavamizi katika kisa hicho walikuwa vijana kutoka eneo jirani la Mayendit na Koch.

Taker amesema wale waliofariki ni raia 10 upande  uliovamiwa na 18 kwa wale waliovamia, kwa kwamba uvamizi huo ulidumu kwa muda tangu siku ya jumapili hadi jumatatu.

Mwezi wa pili mwaka huu watu wengine 72 waliuawa eneo hilo kutoka na vita vya kikabiliwa kwa mjibu wa ripoti ya umoja wa mataifa.

Eneo la Leer ni moja ya maeneo nchini Sudan Kusini, ambayo yalishuhudia janga la binadamu kati ya mwaka 2013 – 2018 wakati wa vita wenyewe kwa wenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.