Pata taarifa kuu
KENYA-KILIMO

Changamoto za wakulima wa Parachichi / Avocado nchini Kenya

Nchini Kenya, baadhi ya wakulima wa parachichi au Avocado, wamo katika njia panda ya ni wapi watauza mazao yao baada ya bodi inayosimamia kilimo cha butsani nchini humo Horticulture Crops Directorate, kusitisha uuzaji wa aina Fulani ya matunda hayo nchini Ulaya.

Mkulima wa Avocado katika Kaunti ya Muranga nchini Kenya
Mkulima wa Avocado katika Kaunti ya Muranga nchini Kenya © AFP - Kevin Midigo
Matangazo ya kibiashara

Hillary Ingati amezuru eneo la Mlima Kenya, mkoa unaongoza kwa kilimo cha tunda hilo na  kutuandalia ripoti hii:-

Muranga, kilomita 72 kutoka jiji kuu la Nairobi, Eneo linaloongoza kwa kilimo cha parachichi, likifuatiwa kwa karibu na kaunti za  Kiambu, Nakuru, Kisii, Nyamira, Meru na  Bomet.

Fredrick Kinyanjui Njuguna, amefanya kilimo cha Avoacdo tangu mwaka wa elfu moja mia tisa tisaini na tisa 1999.

 “Serikali inafaa kufunga kabisa kwa sababu wale watu wako makini  wakulima wa avocado wanaharibiwa na wale waliingia sokoni juzi kwa sababu ya kupenda pesa”

Kilomita chache kutoka Kwa boma lake Mzee Kinyanjui, tunakutana naye Geofrey Gitau, shambani mwake Matunda ya Avocado yanakaribia kukoma ila anawasiwasi.

”Sasa mimi hata sielewi mahali ntapeleka sina ni ule mtu ambaye atakuja shauri kama hatusafirishi nje ya nchi itakuwaje ? Familia yangu hatuwezi kula yote tukayamalizika ”

 

01:54

1 HILLARY INGATI KUHUSU UKULIMA WA Parachichi nchini Kenya E

 

Mary Mwangi Mkulima mwengine  anakiri kuwepo kwa changamoto katika ukulima huu.

 “Ningesema kama tungepata watu wakutuelimisha ile inatakiwa sokoni  watuelekeze vizuri hiyo inaweza kuwa sasa, sababu kama hatuna mafunzo ya kutosha ndio maana ile tunatoa ndio tunapeleka saingine wanakata”

Ni nini kimechangia katika mzozo huu kati ya wakulima wa avocado nchini kenya na soko la ulaya? Lawrence Muriuki mtaalam wa kilimo hiki anaeleza.

 “Siku hizi kuna wengine wanajiita mawakala  na  wakiona upande mmoja umeaanza kuuza parachichi,wanakwenda upande mwingine na kuharibu soko letu kwa sababu wananunua matunda ambayo hayajakomaa ”

 

02:00

2. HILLARY INGATI KUHUSU UKULIMA WA PARACHICHI NCHINI KENYA

Kwa sasa wakulima hawa wanazidi kusubiri ni lini makataa haya yataondolewa wakati huu wanaposubiri shughuli ya uvunaji kuaanza mwezi Machi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.