Pata taarifa kuu
UGANDA-ULINZI

Uganda: Wabunge wakataa kuidhinisha kutolewa kwa pesa kwa jeshi nchini DRC

Siku ya Jumanne, Kamati ya Bajeti ya Bunge ilizuia ombi la ufadhili wa kijeshi. Pesa hizi zilikusudiwa kwa operesheni ya kijeshi ya jeshi la Uganda mashariki mwa Kongo iitwayo Shujaa.

Makao makuu ya Bunge la Uganda.
Makao makuu ya Bunge la Uganda. CC/Andrew Regan
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao waliingia rasmi DRC tarehe 3 Desemba kukabiliana na kundi la waasi wa Uganda wa ADF. Lakini Wizara ya Ulinzi haikushauriana na wabunge kabla ya operesheni hiyo, na kukasirisha wabunge ambao waliona kuwa ni dharau.

Wabunge hawakufurahia hata kidogo kuambiwa tukio ambalo lilitekelezwa kabla wakati wanajeshi wa Uganda walipoingia DRC. Kwa hiyo siku ya Jumanne, wawakilishi wa wizara ya Ulinzi walipokuja kuwaomba dola milioni 26 kufadhili Operesheni ya jeshi mashariki mwa DRC iitayo Shujaa, wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge walionyesha kutokubaliana na hilo.

“Bunge bado linasubiri maelezo. Na hapo unatuomba milioni 26. Lakini kwa msingi gani? Kwangu mimi ni lazima tuzuie hizi pesa hadi tupate taarifa. Kuona ubadhirifu huu, kana kwamba ni biashara yao binafsi. Hapana, hapana, hapana na hapana”, alibaini Ibrahim Semujju Nganda, mbunge aliyechaguliwa katika eneo la Kira.

Pesa hizi zingelitolewa kwa minajili ya kununua vifaa vya kijeshi na mawasiliano au mishahara. Lakini wabunge bado wanahoji kuhusu kutoweka wazi kwa operesheni hiyo.

“Bunge limepewa uwezo wa kujua mkakati wa kuondoa wanajeshi wetu kutoka DRC. Lakini, hatujui hata ni wanajeshi wangapi walitumwa huko, wangapi walifariki, au wangapi walikamatwa na magaidi hao,” anasema mbunge wa upinzani John Baptiste Nambeshe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.