Pata taarifa kuu

Kenya: Mwanahistoria Richard Leakey afariki dunia akiwa na umri wa miaka 77

Mwanahistoria na mwanasiasa maarufu duniani Richard Leakey amefariki siku ya Jumapili akiwa na umri wa miaka 77, ofisi ya rais wa Kenya imetangaza.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (katikati) na mwenyekiti wa Shirika la Huduma ya Wanyamapori nchini (KWS) Richard Leakey (kushoto) baada ya mkutano na waandishi wa habari Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi, Kenya, Aprili 30, 2016.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (katikati) na mwenyekiti wa Shirika la Huduma ya Wanyamapori nchini (KWS) Richard Leakey (kushoto) baada ya mkutano na waandishi wa habari Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi, Kenya, Aprili 30, 2016. REUTERS - Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

"Leo alasiri nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Dkt Richard Erskine Frere Leakey, mkuu wa zamani wa Utumishi wa Umma wa Kenya," Rais Uhuru Kenyatta amesema katika taarifa Jumapili jioni.

Richard Leakey, mtoto wa pili kati ya wana watatu wa Louis na Mary Leakey, wanahistoria na wanaakiolojia, alipata umaarufu kwa kugundua dalili zilizosaidia kuthibitisha mageuzi ya binadamu katika Afrika.

Hakuwa na mafunzo rasmi ya akiolojia, lakini alikuwa ameongoza safari katika miaka ya 1970 ambayo ilisababisha uvumbuzi wa kimapinduzi kwenye mabaki ya kwanza ya hominid. Ugunduzi wake maarufu ulianza mwaka wa 1984, wakati wa uchunguzi katika Ziwa Tukana, nchini Kenya, ambapo aligundua mifupa karibu kamili ya Homo erectus, inayoitwa 'mvulana wa Tukana'.

Richard Leakey  aingia katika siasa

Mnamo 1989, aliombwa na rais wa wakati huo, Daniel arap Moi, kuwa mkuu wa Huduma ya Wanyamapori ya Kenya (KWS). Huko aliongoza kampeni kali dhidi ya ujangili wa pembe za ndovu.

Mnamo 1993, ndege yake ndogo ya Cessna ilianguka katika Bonde la Ufa la Kenya. Wakati huo alipoteza miguu yote miwili katika ajali hiyo.

Richard Leakey pia aliingia katika siasa, na kuongoza taasisi kadhaa za kiraia na kwa muda mfupi akaongoza Utumishi wa Kiraia wa nchi hiyo. Mnamo mwaka 2015, licha ya kuzorota kwa afya yake, alichukua uongozi wa KWS kwa muhula wa miaka mitatu, kwa ombi la Rais Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.