Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-PISTORIUS-Sheria

Kesi ya pistorius: Ofisi ya mwendesha mashtaka yajiandaa kukata rufaa dhidi ya hukumu

Kesi ya mwanariadha wa zamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius bado inaendelea.Ofisi ya mwendesha mashataka, imetangaza Jumatatu Oktoba 27,mchana kwamba itakataa rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa dhidi ya Oscar Pistorius

Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014.
Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014. REUTERS/Werner Beukes/Pool
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia kesi iliyodumu miezi saba, mwanariadha wa Afrika Kusini alihukumiwa wiki iliyopita miaka mitano jela kwa mauaji ya mpenzi wake, Reeva Steenkamp, mwezi Februari 2013.

Ofisi ya mwendesha mashitaka hatimaye imetangaza kuwa itakataa rufaa dhidi ya uamzi wa mahakama na hukumu iliyotolewa dhidi ya Pistorius. Wakati wa kesi hiyo ikisikilizwa, mwendesha mashtaka aliomba Mahakama kutambua kosa la mauaji kwa kukusudia alilofanya Oscar Pistorius.

Kwa mujibu wa Gerrie Nel, Pistorius na mpenzi wake Reeva walihasimiana kabla ya tukio hilo kutokea. Lakini jaji alibaini kwamba mwanariadha huyo alikuwa hana nia ya kuua wakati alifyatua risasi kupitia mlango wa bafuni, ambapo alikuwa mpenzi wake. Pistorius hakupatikana na hatia ya kuua kwa makusudi.

Mwendesha mashtaka aliomba hukumu ya kifungo cha miaka 10 jela. Kwa mujibu ya wanasheria wa mwanariadha huyo, Pistorius anaweza kufanya tu miezi kumi jela na baadae akaondolewa jela na kupewa kifungo cha nyumbani. Mwendesha mashataka amebaini kwamba atawasilisha barua ya kukata rufaa mwishoni mwa wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.