Dunia bado inasubiri kufahamu kilichosababisha kuanguka kwa ndege ya abiria ya Malaysia iliyoanguka juma lililopita na kusababisha vifo vya zaidi ya abiria 200.Ukraine imewatuhumu wapiganaji wanaoiunga mkono serikali ya Urusi kuiangusha ndege hiyo lakini hilo halijathibitishwa wakati huu uchunguzi wa Kimataifa ukiendelea.Lakini je, ni nani anayehusika na njama za kuiangusha ndege hiyo ?Tunajaribu kuchanganua suala hili tata, Emmanuel Makundi anazungumza na wachambuzi wa siasa za Kimataifa Brian Wanyama na Abdulkarim Atiki.