Pata taarifa kuu
Darfour - Uasi

Waasi wa Darfour waendelea kuwa tishio la amani kwa wananchi

Waasi wa Sudani katika Jimbo la Darfour wanaelezwa kuwatishia amani wananchi wa Mji wa El Facher, mji mkuu wa jimbo la Darfour Kaskazini magharibi mwa Sudani, eneo linalo shuhudiwa machafuko tangu miongo kadhaa.

jeep la jeshi la Sudan iliotekwa na waasi
jeep la jeshi la Sudan iliotekwa na waasi RFI/Stéphanie Braquehais
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wananchi wakaazi wa mji huo wa El Facher waasi katika eneo hilo wamekuwa kitisho kikubwa cha amani na usalama ambapo wamekuwa wakishuhdiwa huku na kule mjini hapo wakiwa na silaha na magari ya kijeshi wakitembea kwa mwendo kasi huku wakipga honi huku na kule.

Mji wa Darfour unashudiwa machafuko tangu mwaka 2003 kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaotaka ugavi wa mali asili ya eneo hilo na serikali ya Kharthoum pamoja pia na kupewa sehemu ya Madaraka na serikali.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba kwa kipindi cha mwaka mmoja, machafuko hayo yaligharimu maisha ya mamia ya watu, huku zaidi ya watu milioni mbili wakiliazimika kuyahama makaazi yao, na sasa vitendo vya ujambazi na mapigano ya kikabili kuwania ardhi na visiwa vya maji na machimbo ya madini yakiongezeka.

Mohamed Ibn Chambas mkuu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika jijini Darfour Minuad, amesema Watu zaidi ya laki mbili wamehamishwa makwao katika kipindi cha mwaka mmoja.

Mashahidi wanasema mji wa al Facher inakumbwa na hali ya usalama mdogo ambapo waasi wanavurumisha silaha hewani, hususan asubuhi, na wananchi wanalalama kutohudhuria sala ya alfajiri kwa kuhofia kupigwa risase na waasi hao ambao wanasadikiwa kuwa ni wakundi linalo unga mkono jeshi la serikali ya Sudani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.