Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-Mazungumzo

Vyama vya Upinzani Khartoum vyadai Uhuru na haki

Jeshi la polisi nchini Sudan limetumia gesi ya kutoa machozi kuwatanya waandamanaji wa vyama vya upinzani jana usiku mwandishi wa habari wa AFP ameripoti licha ya serikali ya nchi hiyo kutoa wito wa mazungumzo ya kitaifa.

Wawakilishi  wa vyama vya upinzani wakiwemo kundi dogo la kikomunist na vyama vya congress walijitokeza barabarani huko mji wa kaskazini Khartoum
Wawakilishi wa vyama vya upinzani wakiwemo kundi dogo la kikomunist na vyama vya congress walijitokeza barabarani huko mji wa kaskazini Khartoum AFP
Matangazo ya kibiashara

Takribani wawakilishi mia mbili wa vyama vya upinzani wakiwemo kundi dogo la kikomunist na vyama vya congress walijitokeza barabarani huko mji wa kaskazini Khartoum wakiimba kwa sauti ya juu ''Uhuru na haki''.

Polisi walitumia risasi za mpira na gesi ya kutoa machozi dhidi ya kundi la waandamanaji ambao walitawanyika huku wakiwarushia askari mawe.

Wanachama wa upinzani waliandamana baada ya mkutano katika makao makuu ya chama cha Sudan Congress kujadili hali ya mambo nchini humo ikiwemo uasi, umaskini na mgogoro wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.