Pata taarifa kuu
SYRIA-Uchaguzi

Lakhtar Brahimi aituhumu serikali ya Syria kujaribu kukwepa mazungumzo

Msuluhishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria Lakhtar Brahimi ameionya serikali ya Syria juu ya hatuwa iliopasishwa na bunge la nchi hiyo ya kuandaa uchaguzi huku wapizani wakiwekwa kando. Uchaguzi huo umepangwa kufanyika kati ya mwezi Mei au Juini katika tarehe ambayo haikutajwa rasmi na serikali ya Syria.

Lakhtar Brahimi,  msuluhishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria.
Lakhtar Brahimi, msuluhishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu katika mgogoro wa Syria. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Brahimi ameshauri kuwa mazungumzo ni muhimu kabla ya kufikia kwenye hatuwa hiyo.

Tayari rais Bashar al Assad ameonyesha nia yake ya kuwania uchaguzi huo, jambo ambalo wanadiplomasia wa magharibi wanaokuwa itahatarisha zaidi usalama wa taifa hilo.

Lakhtar Brahimi amesema mchakato huo wa uchaguzi utasababisha kukwamishwa kwa mazungumzo ya waasi na serikali.

Akiulizwa kuhusu uchaguzi huo, balozi wa Syria kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa Bachar Jaafari, amesema hatma ya Syria ipo mikononi mwa wananchi wa Syria.

kulingana na sheria mpya iliopasishwa jana na bunge la Syria, mgombea kwenye uchaguzi wa rais anatakiwa kuwa ameishi nchini Syria kwa kipindi cha miaka kumi iliopita. Hatuwa ambayo inakuja kuwabana wapizani wa Serikali wanaoeshi nje ya taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.