Pata taarifa kuu
UKRAINE

Marekani yaionya Urusi kuingilia kijeshi nchini Ukraine

Marekani imeonya kuwa Rais Barack Obama na viongozi wengine wa Ulaya wanaweza kuahirisha kufanya mkutano wa mataifa yaliyoendelea kiviwanda duniani G8 mjini Sochi Urusi, ikiwa nchi hiyo itaingilia uhuru wa Ukraine.

Rais wa Marekani Barack Obama,
Rais wa Marekani Barack Obama, REUTERS/Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Rais Obama ameelezea kuguswa kwake na ripoti kwamba majeshi ya Urusi yamewasili mjini Crimea, kufuatia madai ya afisa mmoja mjini Kiev kuwa huenda mji huo ukatekwa hivi karibuni..

Aidha rais Obama amesema atasimama pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kuhakikisha kwamba kutakuwa na gharama kwa uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Ukraine, ikiwa ni pamoja na kuuondo amkutano wa G8 mjini Sochi mwezi Juni mwaka huu.

Askari wenye silaha wakiwa wamevalia sare zisizo na alama ya utambulisho wa kitaifa na hakuna alama ya taifa wameonekana karibu na majengo ya serikali na uwanja wa ndege katika mji wa Crimea wa Simferopol, huku afisa wa Ukraine akiituhumu Urusi kwa shambulizi la wazi.

Hata hivyo Urusi imepinga madai hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.