Pata taarifa kuu
NIGERIA-Usalama

Watu 43 wauawa nchini Nigeria: Kundi la Boko Haram lanyooshewa kidole

Watu wanaodhaniwa kuwa ni wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wametekeleza shambulio kwenye shule moja ya sekondari katika jimbo la Yobe na kuua wanafunzi zaidi ya 43. Watu wenye silaha wanadaiwa kuvamia usiku wa juzi kuamkia jana shule iliyoko kwenye mji wa Buni Yadi kaskazini mwa Nigeria na kuanza kuwashambulia kwa risasi wanafunzi waliokuwa wamelala kwenye vyumba vyao na kisha kutokomea kusikojulikana.

Moja kati ya vyumba vya shule moja ya sekondari katika jimbo la Yobe, nchini Nigeria, walikouawa wanafunzi 43.
Moja kati ya vyumba vya shule moja ya sekondari katika jimbo la Yobe, nchini Nigeria, walikouawa wanafunzi 43. AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili limeibua hasira miongoni mwa wananchi ambao wanaona kuwa Serikali imeshindwa kuwalinda dhidi ya mashambulizi ya Boko Haram ambayo siku za hivi karibuni yameendelea kuongezeka yakilenga makazi ya watu.

Rais Goodluck Jonathan amelaani shambulio hilo na kuagiza wanajeshi zaidi kupelekwa kwenye maeneo yaliyoshuhudiwa machafuko zaidi huku akisisitiza jeshi lake kuwadhibiti wapiganaji hao.

Serikali ya Nigeria imetolea wito jana mataifa jirani yaliyokua chini ya ukoloni wa Ufaransa magharibi mwa Afrika, hususan Cameroon kuisadia kukabiliana na kundi la Boko Haram ili kuepusha isiharibu maslahi ya Ufaransa.

“Ninadhani tunahitaji ushirikiano wa kimataifa na wafaransa, pamoja na mataifa yanayozungumza kifaransa katika kanda ya afrika magharibi, hasa kushirikiana kwa pamoja ili kutafutia suluhu tatizo hili kabla halijawa tatizo sugu kwa Ufaransa, na mataifa ya magharibi katika ukanda wa Afrika ya magharibi”, amesema waziri wa habari Labaran Maku.

Tangazo hili linatolewa kabla ya mkesha wa ziara ya rais wa Ufaransa, François Hollande, nchini Nigeria, alhamisi na ijumaa, ambapo François Hollande, atakua mgeni wa heshima katika sherehe za kumbukumbu ya miaka mia moja ya muungano wa taifa hilo.

Nigeria ilifunga juma liliyopita sehemu moja ya mpaka wake iliyoko kaskazini mashariki na Cameroon, katika jimbo la Adamawa, moja kati ya majimbo matatu yanayokabiliwa na mashambulizi ya makundi yenye silaha, likiwemo kundi la Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.