Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-UN

Umoja wa Mataifa unajiandaa kuwatuma wanajeshi wa ziada nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anasema wanajeshi zaidi wa kulinda amani wanastahili kutumwa nchini Jamahuri ya Afrika ya Kati ili kulinda amani na kuzuia makabiliano ya kidini yanayoendelea kushuhudiwa nchini humo. Moon amewaambia wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuwa wanajeshi elfu tatu wanahitajika kwa haraka nchini humo ili kuwalinda raia wanaoendelea kuteseka.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon RFI
Matangazo ya kibiashara

Aidha, ameweka mikakati yake ya kiusalama na kumsaidia rais Catherine Samba-Panza kushughulikia maswala ya Usalama na kibinadmau nchini humo.

Tayari Umoja wa Mataifa umesema kuwa utatuma wanajeshi wake elfu moja nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kujiunga na zaidi ya wanajeshi elfu mbili wa Ufaransa na wale wa Umoja wa Afrika wapatao elfu sita wanaolinda amani nchini humo.

“Raia wa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati hawawezi kusubiri miezi yote hio, ni lazima kikosi hicho kitumwe haraka sana, ili kukinga hali mbaya, ambayo inaweza ikatokea wakati wowote ule”, amesema Ban.

Amebaini kwamba kuna hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo “kuna fununu za kuligawa taifa hilo, na kukimbia kwa watu kutoka jamii ya waislamu kaskazini mwa nchi kwa kuhofia vitisho vinaendeshwa na wanamgambo wa kundi la wakristo la anti-balaka dhidi ya waislamu”, amesema Ban.

Tchad imefahamisha jana kwamba imekamilisha zoezi la kuwarejesha nyumbani raia wa nchi hio waliyokua wakiishi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Tangu mwezi wa desemba mwaka jana mamia kwa maelfu ya raia kutoka jamii ya waislamu, wakiwemo raia kutoka Tchad walikimbia wakihofia usalama wao kutokana na machafuko ambayo yanaendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa sasa, viongozi wa Umoja wa Ulaya wako tayari kutuma wanajeshi, na wanatazamia kuwa operesheni hio ianze mwanzoni mwa mwezi machi, lakini mataifa mengi barani Afrika hayajakua tayari kutuma wanajeshi wao nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.