Pata taarifa kuu
UKRAINE-Upinzani

Upinzani nchini Ukraine wamuomba kansela wa Ujerumani kuwapatishia msaada wa kifedha.

Upinzani nchini Ukraine umeiomba serikali ya Ujerumani kuwapa msaada wa kifedha na kuiadhibu serikali ya rais Viktor Ianoukovitch , na washirika wake kwa kile wanachokisema kuwa inaendelea kukuza unyanyasaji wa kisiasa licha ya kukubali utekelezwaji wa mpango wa msamaha kama walivyoafikiana.

Viongozi wa upinzani nchini Ukraine wa kiwa pamoja na kansela wa Ujerumani Angela Merkel, mji Berlin, 17 februari mwaka 2014
Viongozi wa upinzani nchini Ukraine wa kiwa pamoja na kansela wa Ujerumani Angela Merkel, mji Berlin, 17 februari mwaka 2014 RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika Mazungumzo yao na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin
Upinzani huo uliitaka serikali hiyo ya ujerumani kuzingatia madai waaliyokuwa wamependekeza huku Merkel akisema kuwa itabidi Umoja wa Ulaya kukutana katika mkutano wa dharura kujadili suala zima la Ukraine, Katika Siku za hivi karibuni.
 

“Nina imani kwamba Umoja wa Ulaya na Ujerumani wana mpango wa kuuchukulia vikwazo utawala wa Viktor Ianoukovitch” amesema Vitali Klitschko gwiji wa zamani ndondi aliejinyakulia sifa nyingi nchini Ujerumani, ambae pia ni mmoja kati ya viongozi wa upinzani wa Ukraine katika kikao na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin.

Vitali Klitschko na Arseni Iatseniouk, ambaye ni mshirika wa karibu wa mmoja wa wapinzani anae ziwiliwa, Ioulia Timochenko, wamepokelewa jana kwa mazungumzo na bi Merkel wakati maandamano yakiendelea kushuhudiwa nchini Ukraine, na kusababisha kuendelea kwa mzozo wa kisiasa.

“Hali inaendelea kua mbaya zaidi nchini Ukraine”, amesema bi Merkel, huku akitolea wito utawala wa Viktor Ianoukovitch kuunda serekali ya umoja na kuendelea na mchakato wa kurekebisha baadhi ya vipengele vya katiba ambavyo vinawakandamiza wapinzani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.