Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-Mazungumzo

Umoja wa Mataifa umeomba utaratibu uzingatiwe nchini Syria ili Mashirika yake yaendeshe shughuli za kutoa misaada kwa raia

Hali ya kibinadamu inaendelea kua mbaya kadri siku zinavyoenda nchini Syria. Hio ni tathmini ya mkuu wa shirika la missada la Umoja wa Mataifa Valterie Amos mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Valerie Amos amelitaka Baraza la Usalama la umoja huo kuchukua hatua za haraka kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafikia walengwa kwa wakati kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mapigano.

Valerie Amos, mkuu wa shirika la missada la Umoja wa Mataifa
Valerie Amos, mkuu wa shirika la missada la Umoja wa Mataifa UN Photo/Eskinder Debebe
Matangazo ya kibiashara

Valerie Amos amesema haikubaliki kuona serikali ya Damascus na makundi ya waasi yanaendelea kukiuka sheria kwa kukwamisha ufikishwaji wa misaada ya kibinadamu, huku akikiri kuwa changamoto bado ni katika zoezi hilo.

Takriban watu 1,400 waliondolewa katika mji mkongwe wa Homs tangu ijuma ya juma liliyopita. Mji wa Homs bado unashikiliwa na waasi wa Syria, lakini umezingirwa na jeshi la Syria linalomuunga mkono rais wa Syria Assad.

Kwa mujibu wa mkuu wa mji wa Homs, zoezi la kuwaondoa raia waliyokwama katika mji huo litaendelea kwa siku tatu mfululizo tangu hii leo ijumaa.

Wakati huo huo majadiliano baina ya wajumbe wa serikali ya Damascus na wapinzani yameendelea mjini Ganeva Uswisi, pande zote zimeendelea kutofautiana juu ya ajenda za mazungumzo.

Mpatanishi wa mgogoro huo Lakhdar Brahimi amesema mazungumzo hayo bado yana changamoto kubwa na itakuwa vigumu kusonga mbele bila kuafikiana.

Lakhdar Brahimi atatakiwa kutumia uwezo wake wote ili kuzishawishi pande zote mbili zifikiye makubaliano.

Mazungumzo kati ya wajumbe wa serikali ya Damascus na wale wa upinzani yanatarajiwa kuanza tena leo ijumaa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.