Pata taarifa kuu
IRAQ-Marekani-Usalama

Waziri mkuu wa Iraq anyooshewa kidole cha lawama na wajumbe wa baraza la wawakilishi nchini Marekani

Wajumbe wa baraza la wawakilishi nchini Marekani wamemtuhumu waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki kwa kuchangia kuendelea kwa mashambulio ya kujitowa muhanga yanayoendelea kushuhudiwa nchini Iraq kufuatia kutoharakisha mpango wa kudumisha maridhiano baina ya wananchi wa taifa hilo.

Waziri mkuu wa Iraq, Nuri al Maliki
Waziri mkuu wa Iraq, Nuri al Maliki RFI
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa baraza hilo wanaohusika na maswala ya kigeni wamemuhoji Brett McGurk afisaa kwenye wizara ya mambo ya nje wa Marekani anaye husika na maswala ya Iraq kuhusu kitisho cha makundi ya Alqaeda na makundi ya kisunni yenye msimamo mkali hususan kundi la EIIL.

Iraq imetumbukia katika dimbwi la machafuko tangu mwanzoni mwa mwaka 2013 na ambapo watu zaidi ya elfu moja wameripotiwa kupoteza maisha katika mwezi januari pekee. Hapa jana kumeshuhudiwa pia mashambulia matatu ya kujitowa muhanga yaliosababisha vifo vya watu 33 na kuwajeruhi wengine zaidi ya ishirini.

Inaarifiwa kuwa kundi la Alqaeda linatekeleza mashambulio 40 kwa mwezi. Mkuu wa kamisheni ya wajumbe wa baraza hilo Ed Royce amemyooshea kidole cha lawama waziri mkuu wa serikali na kumtaka kuwa na uwezo wa kuiongoza Iraq kuondokana na hali hiyo ya machafuko.

Hayo yanaarifiwa wakati huu kundi la Alqqeda likiendelea kujizatiti nchini humo ambapo wataalamu wanasema kundi hilo linatumia fursa ya mzozo wa kimadhehebu ya wasunni waliowachache nchini Iraq na Wasunii waliowengi katika kuendeleza mashambulizi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.