Pata taarifa kuu
THAILAND-Maandamano

Thailand : Waandamanaji waapa kusitisha maandamano

Waandamanaji wamepinga kuondoka barabarani nchini Thailand na kuahidi kuiangusha serikali baada ya kufanyika kwa uchaguzi uliosusiwa na upinzani na tayari Marekani imetahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mapinduzi. Mamia ya waandamanaji wamejiunga na mwanaharakati Suthep Thaugsuban na kuthibtisha kuwa uchaguzi uliofanyika hauwezi kamwe kusitisha dhamira yao ya kuungausha utawala wa waziri mkuu Yingluck Shinawatra ambaye anatuhumiwa kuwa kibaraka wa kaka yake Thaksin Shinawatra aliye kimbilia uhamishoni.

Suthep Thaugsuban, Kiongozi mkuu wa wandamanaji, wakati wa maandamano mjini Bangkok nchini Thaïlande, januari 19 mwaka 2014.
Suthep Thaugsuban, Kiongozi mkuu wa wandamanaji, wakati wa maandamano mjini Bangkok nchini Thaïlande, januari 19 mwaka 2014. PORNCHAI KITTIWONGSAKUL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku kadhaa baada ya kufanyika kwa uchaguzi, tume ya uchaguzi nchini humo haijatowa hata matokeo ya muda kufuatia vurugu za maandamano zinazoendelea ambapo waandamannaji wamezuia shughuli za usafirisha wa karatasi za kupigia kura na kusababisha takriban vituo elfu kumi kufungwa.

Hata hivyo tume inayoandaa uchaguzi ilitowa takwimu za idadi ya watu walioshiriki zoezi hilo la upigaji kura ambapo aslimia 45.9 kati ya watu milioni 44.6 waliojiorodhesha ndio walioshiriki.

Kulingana na mtaalamu wa siasa katika chuo kikuu cha Bankok Janjira Sombatpoonsiri amesema Idadi hiyo imekuwa ndogo kufuatia hofu ya wananchi ambao wengi hawakwenda kupiga kura kutokana na hofu na hivo kusalia majumbani.

Serikali ya Marekani imetahadharisha nchi hiyo juu ya kutokea kwa mapinduzi ya kijeshi ambayo mara kadhaa yamekuwa yakishudiwa.

Upinzani nchini unapinga kufanyika kwa uchaguzi huo na tayari umesema utapeleka kesi mahakamani kutaka uchaguzi huo ufutwe.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.