Pata taarifa kuu
MALI-Mazungumzo

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umeyapokea kwa mazungumzo makundi ya waasi nchini Mali

Leo ni siku ya pili ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ukiendelea na ziara yake nchini Mali. Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliowasili mjini Bamako mwishoni mwa juma lililopita kwa ziara ya siku mbili unatarajiwa kutamatisha ziara hiyo hii leo nchini Mali.

Wawakilishi wa makundi ya waasi mjini kaskazini mwa Mali wakipokelewa kwa mazungumzo na ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Wawakilishi wa makundi ya waasi mjini kaskazini mwa Mali wakipokelewa kwa mazungumzo na ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa RFI
Matangazo ya kibiashara

Ujumbe huo unaoundwa na mabalozi kumi na tano, ambao waliutembelea jana mji wa Mopti, ambapo walikukutana na rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, kwa mazungumzo kuhusu mchakato wa amani kaskazini mwa nchi hiyo unaoonekana kusuasua.

Mazungumzo kati ya utawala na makundi ya waasi wa kaskazini yanapaswa yaanzishwe, hata kama hayajaanza. Wawakilishi wa makundi ya waasi kaskazini mwa Mali wamepokelerwa leo kwa mazungumzo na ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Makundi hayo hayajajiunga pamoja, lakini madai yao ni kama yanafanana.

Gerard Arault balozi wa Ufaransa Kwenye Umoja wa Mataifa na kiongozi mkuu wa Ujumbe huo, amesema.

“Rais wa mali anatamani kuwa na mazungumzo na wananchi wote wa Mali, na ninaposema wananchi wote sio tu vikundi vya waasi lakini pia raia wa kawaida.

Kwanza rais ametuhakikishia kuwa lengo lake ni kufanya mazungumzo na si malumbano, anatamani suluhu iwe ya kisiasa na kujifunza kutokana na yaliyopita na hasa amani ya kudumu”, amesma Gerard Arault.

Ujumbe huo umewasili mjini bamako wakati taarifa za hivi karibuni zinabaini kudorora kwa mahusiano baina ya Serikali ya Mali na Uongozi wa vikosi vya kimataifa nchini humo, Minusma.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.