Pata taarifa kuu
SYRIA-Mazungumzo

Serikali ya Damascus yaruhusu raia wa kawaida kuondoka katika mji wa Homs

Baada ya siku mbili ya mazungumzo kuhusu raia wanaoziwiliwa katika mji wa Homs kati ya ya wajumbe wa serikali ya Syria na wale wa waasi mjini Geneva, hatimaye serikali ya Syria inasema sasa inawaruhusu watoto na wanawake kuondoka katika mji wa Homs ambao umekuwa chini ya ulinzi wa majeshi ya serikali kwa zaidi ya miezi 18 sasa.

Katibu mkuu wa UN  Ban Ki-moon, akiwa na wajumbe kutoka pande mbili zinazozozana nchini Syria  kwenye mkutano wa Geneva kuhusu Syria
Katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon, akiwa na wajumbe kutoka pande mbili zinazozozana nchini Syria kwenye mkutano wa Geneva kuhusu Syria RFI
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umetolewa na Damascus wakati wa mazungumzo ya amani kati yao na upinzani mjini Geneva nchini Uswisi na kutangazwa na mpatanishi wa Kimataifa Lakdhar Brahimi.

Tangazo hilo linasema kwamba wanawake na watoto wako huru kufanya shughuli zao katika mji wa Homs, na wanaweza wakaondoka na kuingia katika miji mingine ya nchi ya Syria.

Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Syria Faisal Mekdad amesema wanawake na watoto wako huru kuondoka katika mji huo ambao umekuwa ukishuhudia mapigano kati ya wanajeshi na waasi, lakini makundi ya wapiganaji yanawazuia kuondoka.

Upinzani umekubali kuipa serikali idaidi ya watu wanaozuiliwa na makundi ya wapiganaji.

Lakdhar Brahimi amesema kuwa mazungumzo hayo yanaendelea kwa mwendo wa kinyonga na leo Jumatatu wajumbe wa serikali na upinzani wanatarajiwa kutoa mwelekeo wa mazungumo haya ya amani, kukizingatiwa vigezo vitakavyotumiwa kwa uundwaji wa serikali ya mpito.

Swala la uundwaji wa serikali ya mpito linaonekana kuleta utata kati ya upinani wa rais Bachar a-Assad na wafuasi wake.

Hata baadhi ya mataifa ya ulaya, Marekani, Asia na Mashariki ya Kati yametafautiana kuhusu uundwaji wa serikali hio ya mpito.

Upinzani nchini Syria na washirika wake kama vile mataifa ya kimagharibi na tawala za kifalme za mataifa ya Ghuba yanashinikiza kwamba Bachar asishirikishwi kwenye serikali hio, madai ambayo yanatupiliwa mbali na serikali ya Damascus pamoja na Urusi na Iran, mataifa ambayo yanamuunga mkono Bachar al-Assad.

“ Leo tunaanza kuzungumzia swala la uundwaji wa serikali ya mpito, ikimaanisha kua ni mageuzi kutoka utawala wa kiimla kwenda utawala utakaochaguliwa chini ya mfumo wa vyama vingi, amesema Louai Safi, mmoja kati ya wajumbe wa upinzani masaa machache kabla ya kuanza kikao cha siku ya tatu ya mazungumzo, akiiomba serikali kukubaliana nao kupitia suluhu ya kisiasa kuliko kuendelea na mapigano.

Mapigano nchini Syria yamesababisha watu 130,000 kupoteza maisha na mamilioni kuyahama makaazi yao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.