Pata taarifa kuu
UKRAINE-Maandamano

Upinzani nchini Ukraine umeapa kuendelea na maandamano

Upinzani nchini Ukraine umetoa saa ishirini na nne kwa utawala wa nchi hiyo kuitisha uchaguzi mkuu, ama nchi hiyo ijiandae kwa maandamano makubwa zaidi.Kauli ya upinzani imetolewa saa chache baada ya viongozi wake kuwa na mazungumzo na raia wao, na kumtaka rais Viktor Yanukovich kuitisha uchaguzi mkuu mwingine ili kunusuru taifa hilo kutumbukia kwenye machafuko zaidi.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la upinzani limetolewa wakati huu kukiripotiwa maandamano zaidi mjini Kiev ambapo watu watano wameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi wakati wakikabiliana na polisi wa kutuliza ghasia.

Hapo jana serikali ya nchi hio ilianza utekelezaji wa sheria yake inayokataza maandamano kwenye sehemu za umma sheria ambayo imewafanya waandamanaji kuwa wagumu zaidi kuondoka kwenye maeneo ambayo wanayakalia kwa sasa.

Waziri mkuu wa taifa hilo, amesisitiza kuwa kile kinanchofanywa na upinzani kinaenda kinyume na matakwa ya katiba ya nchi hiyo ingawa amekiri kuwa serikali yake huenda ikatekeleza matakwa ya upinzani kuitisha uchaguzi mwingine.

Rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch aliwatolea wito wananchi wake jana kutoshirikiana na wabaguzi wanaochochea machafuko katika mji mkuu wa taifa hilo wa Kiev yaliosababisha vifo vya watu zaidi ya wanne.

Katika taarifa iliotolewa na ikulu ya rais Viktor Ianoukovitch amebaini maskitiko yake kuhusu vifo vya watu zaidi ya wanne vilivyosababishwa na vurugu zinazo chochewa na wabaguzi na kuwatolea wito wananchi wake kutoshirikiana na wachochezi wanaolenga kuharibu hatuwa zilizofikiwa na serikali yake.

Upinzani nchini Ukraine umeapa kuendelea na maamdano hadi kuungusha utawala wa Ianoukovitch, wakati huo huo naye akiapa kung'atuka madarakani.

Umoja wa Mataifa umelani namna polisi imetumia nguvu na kuwafyatulia risase waandamanaji.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.