Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Siasa

Hali ya usalama imeanza kurejea jijini Bangui wakati huu rais mpya wa kipindi cha mpito akitarajia kuapishwa kesho alhamisi

Rais mpya wa kipindi cha mpito nchini jamhuri ya Afrika ya kati ambaye anatarajiwa kuapishwa baadaye alhamisi hii, amepania kilipa kipao mbele swala la vijana wanaoibukia kushika silaha na ambalo limekithiri nchini humo,na badala yake amepanga kuwapendekezea shughuli nyingine kwa hatma ya maisha yao.

Catherine Samba-Panza rais mpya wa jamhuri ya Afrika ya kati
Catherine Samba-Panza rais mpya wa jamhuri ya Afrika ya kati RFI
Matangazo ya kibiashara

Hali ya kawaida imeonekana kurejea mchana wa leo jijini Bangui ambapo miendeneo ya huku na kule imeshuhudiwa katika jiji hilo, ambapo kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mchafuko, wananchi wamesema hakuna milio ya risase iliosikika katika usiku wa kuamkia leo jumatano.

Hata hivyo wanajeshi wa Ufaransa waliopo katika operesheni Sangaris na wale wa Afrika wa kikosi cha misca ambao wanalinda maeneo kadhaa nchini himo pamoja na ma mia ya wakimbizi waliokimbia makwao, wameonya kwamba licha ya uteuzi wa Samba Panza kupokelewa kwa mikono miwili na pande zote, suluhu ya mzozo bado haijapatikana.

Akizungumza na wanahabari mjini Bangui hapo jana, rais Catherine Samba-Panza anasema kuwa serikali yake itaundwa na mawaziri 8 ambao uteuzi wake utazingatia namna ambavyo wanaweza kusaidia kuleta mabadiliko nchini humo.

Katika hatua nyingine kumeendelea kuripotiwa mapigano kwenye maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo ambako baadhi ya raia wamekuwa wakitekeleza mauaji ya kulipiza kisasi dhidi ya watu wanaowatuhumu kuua familia zao.

Alexis Mascirialli ambae ni msemaji wa shirika moja la kimataifa la kutoa misaada nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, amesema kuwa bado kumekuwa na uhaba wa chakula kutokana na magari mengi ya misaada kushindwa kufika kwenye maeneo husika kuhofia usalama.

Kufuatia uteuzi wa rais Catherine Samba-Panza, Jumuiya ya Kimataifa imeahidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha amani ya kudumu inarejea nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.