Pata taarifa kuu
IRAQ

Taifa la Iraq lakabiliwa na machafuko ya wao kwa wao huku kujitokeza mgawanyiko baina ya raia kutokana na madhehebu ya kidini

Mapigano makali yameshuhudiwa baina ya vikosi vya serikali ya Iraq na kundi la wanamgambo wanaofungamana na kundi la Al-qaeda ambao wameiteka miji miwili muhimu, hii ikiwa ni changamoto mpya kwa waziri mkuu wa taifa hilo Nuri Al Malik. Baadhi ya waislamu wa dhehebu la wasuni, wanampinga Nuri Al Malik, ambae nae pi ni kutoka dhehebu hilo.

Matangazo ya kibiashara

Polisi katika mji wa Ramadi imesema mapigano yamepungua jioni ya jana baada ya kushuhudiwa makabiliano makali mchana kutwa, huku kukiwa na hali ya mkanganyiko katika mji wa Fallouja, miji ambayo inakaliwa na wafuasi wengi waumini wa madhehebu ya sunni na ambayo imekuwa ikishuhudiwa mara kadhaa maandamano ya kumpinga waziri mkuu Nuri Al Malik, ambaye anatuhumiwa kujilimbikizia madaraka na kuwatupilia watu wa madhehebu ya wa sunni.

Fallouja na Ramadi ni miji ambayo ilikuwa ngome ya upinzani uliopelekea uvamizi wa Majeshi ya Marekani uliomuondowa Madarakani rais wa zamani wa taifa hilo Marehemu Sadam Hussein ambaye alikuwa wa dhebu la wa Sunni mwaka 2003.

Miaka miwili baada ya kuondoka kwa majeshi ya Marekani nchini Iraq Desemba mwaka 2011, taifa hilo linakabiliwa na changamoto kubwa ya kudhibiti hali ya usalama mdogo kufuatia kutoridhika kwa watu wa madhehebu ya wa Wasunni pamoja na vita vya Syria vinavyo changia kuendelea kwa machafuko.

Machafuko haya mapya katika miji ya Fallouja na Ramadi yalianza mwanzoni mwa juma hili, wakati polisi wa Usalama walipoivamia ngome ya wapinzani wa serikali mjini Ramadi.

Juma hili waziri Mkuu Nuri Al Malik alitangaza kuvituma vikosi zaidi katika miji hiyo.

Duru za kijeshi zimeariku kwamba wanajeshi wapo kando ya miji hiyo wakisubiri kupewa idhni wakati wowote itapo hitajika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.