Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-Mazungumzo

Mazungumzo ya kusaka amani nchini Sudan Kusini yaanza mjini Addis-Ababa nchini Ethiopia

Wajumbe wa serikali ya rais wa Sudani Kusini Salva Kiir na wale wa Riek Machar ambae ni makamo wa zamani wa rais wa taifa hilo wapo kwenye mazungumzo ya kutafuta suluhusu ya mzozo ulipo, mjini addis-Ababa, nchini Ethiopia. Duru kutoka jijini Addis Ababa zimesema kuwa wajumbe wa Serikali ya Juba wamewasili jana muda mfupi baada ya wajumbe wa waasi kuwasili kwa ajili ya kuanza mazungumzo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Tendros Adhanom amesema mazungumzo ya awali yanatarajia kuanza leo hii huku mazungumzo rasmi yakipangwa kuanza baada ya pande zote mbili kukutana.

Duru za Umoja wa nchi za pembe ya Afrika na baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki, IGAD zimearifu kwamba wajumbe hao wapo katika hatuwa ya kwanza na watajadili juu ya kufikia makubaliano ya kisitisha vita kabla ya kujadili kuhusu tofauti za kisiasa zilizo sababisha pande moja kuanzisha vita.

Licha ya kuwatuma wajumbe wake jijini Addis Ababa kwa ajili ya kuanzishwa kwa majadiliano na serikali ya Juba, Riek Mashar yeye anasema hayupo tayari kuketi ana kwa ana na Salva Kiir na kwamba mapigano yanaendelea hadi mjini Juba.

Nchi ya Sudan Kusini, inakabiliwa na mapigano toka tarehe 15 mwezi disemba, mapigano ambayo yanachochewa kutokana na malumbano kati ya rais Salva Kiir na aliekua makamo wake, Riek Machar.


Mapigano hayo yamaesababisha maalfu ya watu wanapoteza maisha na wengine laki moja na alfu themanini kuyahama makaazi yao.

Awali Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini, ulilaani katika ripoti yake mauaji yanayoendelea nchini humo baada ya kugundua miili ya raia na wanajeshi waliokamatwa na kuuawa baadae katika maeneo mengi ya taifa hilo.


Umoja huo wa mataifa ulisema unatiwa wasiwasi na hali ya usalama inayoendelea, na ambapo vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vinatekelezwa tangu siku kumi na tano zilizopita.

Kwa sasa Umoja wa Mataifa umepongeza hatua hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.