Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Waasi wa Sudan Kusini wanyooshewa kidole cha lawama kwa mauwaji yaliyotokea katika baadhi ya miji ya nchi hio

Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini,umelaani katika ripoti yake mauaji yanayoendelea nchini humo baada ya kugundua miili ya raia na wanajeshi waliokamatwa na kuuawa baadae katika maeneo mengi ya taifa hilo.Umoja huo wa mataifa imesema unatiwa wasiwasi na hali ya usalama inayoendelea, na ambapo vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vinatekelezwa tangu siku kumi na tano zilizopita.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati viongozi wa Ethiopia wakifahamisha kuwa wajumbe wa makamo wa rais wa zamani Riek Mashar na wale wa rais Salva Kiir wanasubiriwa mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo ya kumaliza machafuko.

Mauaji dhidi ya raia wasiokuwa na hatia na askari walitekwa yameshuhudiwa katika maeneo kadhaa ya nchi kama inavyothibitishwa na ugunduzi wa idadi kubwa ya miili ya watu katika mji mkuu wa Juba, lakini pia katika miji ya Malakal na Bor katika majimbo ya juu ya Nile na Jonglei.

Licha ya kuwatuma wajumbe wake jijini Addis Ababa kwa ajili ya kuanzishwa kwa majadiliano na serikali ya Juba, Riek Mashar yeye anasema hayupo tayari kuketi ana kwa ana na Salva Kiir na kwamba mapigano yanaendelea hadi mjini Juba.

Rebecca Garang, mjane wa John Garang, kiongozi wa zamani wa waasi wa SPLA, ambae ana ushawishi mkubwan ni m'moja wa wanaoshiriki katika ujumbe ambao umetumwa na Riek Machar kuzungumza na rais Salva Kiir mjini Addis-Ababa.

Nchi ya Sudan Kusini inakabiliwa na mapigano toka tarehe 15 mwezi disemba, mapigano ambayo yanachochewa kutokana na malumbano kati ya rais Salva Kiir na aliekua makamo wake, Riek Machar.
Mapigano hayo yamaesababisha maalfu ya watu wanapoteza maisha na wengine laki moja na alfu themanini kuyahama makaazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.