Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-mazungumzo

Waasi nchini Sudan Kusini Waapa Kuendelea na mapigano hata kama mazungumzo yamo mbioni kuanzishwa

Aliekua makamo wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar, ambae ni kiongozi wa kundi la waasi wanaoendesha mapigano kwa muda wa majuma mawili dhidi ya jeshi la serikali, amefahamisha kwamba hatashiriki mazungumzo ya ana kwa ana na rais Salva Kiir, lakini ametuma ujumbe kwa niaba yake mjini Addis-Ababa kuanzisha mazungumzo na serikali ya Juba.

Matangazo ya kibiashara

Machar amesema hatasitisha mapigano haraka, akibaini kwamba suala la kusitisha mapigano linapashwa kupewa nafasi katika mazungumzo.

“Ndio maana ujumbe wangu unaenda Addis-Ababa, ili uzungumziye hili suala”, amesema Riek Machar.

Hayo yakijiri, mapigano yanaendelea mjini Bor, huku waasi wakidai kuuthibi kwa mara nyingine tena mji huo ambao walikua waliupoteza hivi karibuni.

“Jeshi langu linaelekea Mjini Juba (mji mkuu wa Sudan Kusini), hakuna kusitisha mapigano wakati huu”, amesema Machar, akibaini kwamba waasi waliuteka mji wa Bor.

Machar amesema hajawa tayari kukutana uso kwa uso na Salva Kiir.
“ Itatokana na jinsi mazungumzo yatakavyokua yakiendelea”, Ntakutana nae kwa mazungumzo baadae, wakati mazungumzo kuhusu usitishwaji mapigano yatakua yameanza,lakini sidhani kua yatasitishwa hivi karibuni”, amesema Riek Machar.

Riek Machar amefahamisha kwamba haikua nika yao ya kuanzisha vita, bali walilazimishwa kufanya hivo.

Rebecca Garang, mjane wa John Garang, kiongozi wa zamani wa waasi wa SPLA, ambae ana ushawishi mkubwan ni m'moja wa wanaoshiriki katika ujumbe ambao umetumwa na Riek Machar kuzungumza na rais Salva Kiir mjini Addis-Ababa.

Rebecca Garang ni kutoka kabila la Dinka, anakotoka rais Salva Kiir.

Wengine watakaoshiriki ujumbe huo ni Taban Deng Gai, mkuu wa zamani wa mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Unity, ambao sehemu kubwa inashikiliwa na waasi, na Hussein Mar, naibu mkuu wa zamani wa jimbo la Jonglei.

Riek Machar, ameomba kwa mara nyingine ten kuachiliwa huru kwa washirika wake wa karibu wanaoziwiliwa kwa majuma mawili sasa, akiwemo Pagan Amum, aliekua katibu mkuu wa chama kiliyoko madarakani, ambae aliachichwa kazi katika mwezi wa julai.

“Wanapashwa kuwaachilia huru, kwani ninamtegemea Pagan Amum kwa kushirika katika mchakato wa kuanzisha mazungumzo”, amesema Riek Machar.

Nchi ya Sudan Kusini inakabiliwa na mapigano toka tarehe 15 mwezi disemba, mapigano ambayo yanachochewa kutokana na malumbano kati ya rais Salva Kiir na aliekua makamo wake, ariek Machar.

Mapigano hyo yamaesababisha maaflfu ya watu wanapoteza maisha na wengine laki moja na alfu themanini kuyahama makaazi yao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.