Pata taarifa kuu
JAMUHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

Watu 40 wasiojulikana wameuwawa mjini Kinshasa baada ya kujaribu kuteka baadhi ya vituo muhimu vya mji mkuu huo

Waandishi wa habari kutoka Radio na Television vya taifa ( TRNC ) walichukuliwa mateka na vijana wenye silaha Jumatatu asubuhi katika mji mkuu wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kinshasa, ambapo polisi wametumwa ili kuwaondoa wanahabari hao mikononi mwa watekaji nyara, Vyanzo vya polisi vimefahamisha.

Matangazo ya kibiashara

"Ni watu wanaobebelea silaha ikiwa ni pamoja na mapanga na bunduki ambao wamewateka nyara waandishi wa habari.

Operesheni ya kuwaondoa wanahabari hao mikononi mwa watekaji nyara inaendelea, na tayari wahusika wametambuliwa”, amesema kanali Mwana Mputu anaehusika na mawasiliano katika polisi.

Matangazo ya televisheni ya taifa yalikatwa muda mfupi baada ya tukio hilo. Kabla ya watekaji nyara kuvamia jengo hilo, picha zilionyesha watangazaji wawili, ambao walikua wakiendesha kipindi kiitwacho, " Le Panel" , wamekaa, wakiwa na hofu lakini shwari, na nyuma yao kijana akiwatishia, huku akipumua kwa kasi. Watu wengine ambao walipenya ndani ya jengo hilo hawakuweza kuonekana.

Milio ya risasi imesikia, bila hata hivo kufahamu iwapo risasi hizo zimekua zikifyatuliwa na polisi , washambuliaji au ilikua kubadilishana risasi kati ya kambi hizo mbili.

Hofu imetanda mjini Kinshasa. Kazi za usafiri zimesimama,baadhi ya ofisi zimefungwa na raia wamekua wakijiuliza nini kimetokea.

Askari polisi, wanajeshi na wanajeshi wa kikosi maalumu kinacho linda usalama wa rais Joseph Kabila, wamewekwa kila mahali, ikiwemo kwenye jengo la redio na televisheni vya taifa (RTNC) pamoja na makao makuu ya bunge.

Wakazi kadhaa wa mji wa Kinshasa wamesema milio ya risasi imesikia kwa muda wa dakika kadhaa kwenye jengo la redio na televisheni vya taifa (RTNC).

Hata hivo, inasemekana kua milio ya risasi imesikia pia kwenye uwanja wa ndege wa N'jili na karibu, kambi ya kijeshi ya Tshatshi. Hali hio inajiri pia katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Congo wa Lubumbashi, ambapo milio ya risasi imesikika. 

Duru za serikali zinafahamisha kwamba watekaji nyara 40 wameuwawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.