Pata taarifa kuu
JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

Raia wa kigeni waendelea kuondoka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuokoa maisha yao

Mamia ya raia wa Chad waishio nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wameendelea kukimbia wakirejea makwao kutokana na mashambulizi baina ya Wakristo na Wasilamu yanayoendelea kushuhudiwa. Misafara ya raia hao imeonekana ikiondoka mjini Bangui kuanzia siku ya ijumaa chini ya ulinzi wa walinda amani.

REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imechochewa na jamii ya Wakristo ambao wameanza kuwalenga baada ya raia wa Chad na wanajeshi wao waliopo nchini humo wakiwashutumu kuwasaidia wapiganaji wa Seleka ambao ni waislamu.

Sudan nayo imesema itafuata nyayo za Chad na kuwaondoa raia wake takribani 275 kwa ndege leo jumapili, kutokana na usalama kuzidi kuzorota.

Majeshi ya Ufaransa na Afrika yanajitahidi kurejesha usalama uliozorota toka mwezi machi mwaka huu wakati kundi la Seleka lilipochukua madaraka baada ya kumpindua Rais wa zamani Francois Bozize, lakini jitihada hizo zimezidi kupata changamoto.

Umoja wa Mataifa umesema utaharakisha mpango wa kupeleka kikosi chake cha kulinda amani, wakati ikiripotiwa kuwa watu zaidi ya elfu moja wameuawa toka kuanza kwa mapigano makali takribani majuma matatu yaliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.