Pata taarifa kuu
MAREKANI

Edward Snowden asema amefanikisha mpango wake

Aliyekuwa afisa wa Inteljensia nchini Marekani Edward Snowden amesema kuwa lengo lake limetimia baada ya kuvujisha siri za Kiinteljiesia kuhusu namna serikali ya Marekani inavyochunguza mawasiliano ya watu mbalimbali duniani.Miezi sita tu baada ya kuvujisha siri za shirika la usalama la nchini Marekani, Edward Snowden kwa mara ya kwanza amefanya mahojiano na gazeti la Washington Post na kujigamba kuwa mpango wake umekamilika.

DR
Matangazo ya kibiashara

Snowden mwenye umri wa miaka thelathini amesema ameridhika na anajiona mshindi kwa sababu watu na mataifa mbalimbali sasa wameweza kufahamu kuwa Marekani imekuwa ikichunguza kumbukumbu za mawasiliano yao na intaneti.

Snowden aliwasili nchini Urusi mwezi June na kukaa katika uwanja wa ndege kwa zaidi ya mwezi mmoja kabla ya kupatiwa hifadhi wakati akitafuta uwezekano wa kuelekea katika nchi nyingine zilizoonesha nia ya kumuhifadhi.

Bwana Snowden aliondoka Marekani mwishoni mwa mwezi Mei, akichukua kiasi kikubwa cha nyaraka za siri kuhusu mpango wa udukuzi wa Marekani.

Anakabiliwa na mashitaka ya ujasusi nchini Marekani.

NSA iligundulika kuhusika katika udukuzi wa data za simu. Taarifa za kina za watu na taasisi zilizolengwa na udukuzi wa mashirika ya ujasusi ya Uingereza na Marekani zilichapishwa wiki iliyopita na magazeti ya The Guardian, The New York Times na Der Spiegel.

Magazeti hayo yamesema orodha ya watu na taasisi zipatazo 1,000 zilizolengwa ni pamoja na Kamishna wa Umoja wa Ulaya, mashirika ya kibinadamu na maafisa wa Israel akiwemo waziri mkuu.

Makampuni makubwa ya teknolojia ya mawasiliano nchini Marekani ya Google, Microsoft na Yahoo yanachukua hatua ya kuzuia ukusanyaji wa data unaofanywa na serikali yao.

Marekani tayari imeingia katika mzozo wa kidiplomasia na baadhi ya mataifa ikiwemo Ujerumani baada ya kubainika kuwa mawasiliano ya simu ya Kansela Angela Markel nayo yalichunguzwa.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff naye pia alikasirishwa na taarifa kwamba shirika la ujasusi la Marekani, NSA, liliingilia mtandao wa kompyuta wa kampuni ya mafuta ya serikali ya Brazil, Petrobras ili kukusanya taarifa na mawasiliano ya barua pepe na simu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.