Pata taarifa kuu
SYRIA

Watu 76 wauwawa nchini Syria katika mashambulizi ya anga Kaskazini mwa jiji la Aleppo

Mashambulizi ya anga yanayodhaniwa kutekelezwa na vikosi vya serikali ya rais Bashara al-Assad mjini Aleppo, kaskazini mwa Syria yamesababisha vifo vya watu 76 wakiwemo wanawake 4 na watoto 28 wenye umri ulio chini ya miaka 18. Idadi hio imethibitishwa na Shirika linalotetea haki za binadamu nchini Syria SOHR.

REUTERS/Bassam Khabieh
Matangazo ya kibiashara

 

Awali Shirika hilo lilitoa taarifa ya kuuwawa kwa watu thelathini na sita wakiwemo watoto kumi na tano. Taarifa hio haijathibitisha iwapo kuna waasi waliouwawa
Waangalizi wa Haki za Binadamu wanasema mauaji hayo yametokana na mashambulizi yaliyotekelezwa katika wilaya zinazodhibitiwa na waasi.

Mashambulizi hayo yamekuja siku moja baada ya Shirika la Msalaba mwekundu kufikisha msaada wa chakula na dawa katika gereza moja ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa waasi kwa takribani miezi nane.

Vikosi vya serikali vimekuwa vikifanya mashambulizi hayo kuwalenga waasi, lakini hata wale wasiokuwa na hatia wamekuwa wakiathiriwa.

Mamilioni ya raia wa nchi hiyo wameendelea kukimbia makazi yao, huku watu zaidi ya laki moja na ishirini wakiuawa toka kuanza kwa mapigano hayo miezi thelathini na tatu iliyopita.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.