Pata taarifa kuu
KENYA

Kenya yaadhimisha miaka 50 tangu ipate uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza

Wananchi wa Kenya wameadhimisha miaka hamsini ya Uhuru katika sherehe zilizoongozwa na rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta jijini Nairobi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika wakiwemo marais na Mawaziri Wakuu. Maelfu ya watu wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi na kuanza kwa burudani kutoka makundi mbalimbali.

Photo: AP
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa marais waliohudhria maadhimisho hayo ni pamoja na Goodluck Jonathan wa Nigeria, Joyce Banda wa Malawi, Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo, Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Yoweri Museveni wa Uganda na wengineo wengi.

Katiba hotuba yake kwa taifa rais Uhuru Kenyatta ameleezea mafanikio ya kichumi, kisiasa, kielimu na mambo mengine yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita.

Akizungumza na maelfu ya wakenya katika maadhimisho hayo, rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameipongeza Kenya kwa kupiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali na kusisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Kenya katika miaka ijayo kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Naye rais wa Uganda Yoweri Museveni alitumia nafasi hiyo kuyakosoa mataifa ya Magharibi kukataa kusitisha kesi inayomkabili rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto katika Mahakama ya Kimataufa ya ICC na kusema kuwa bara la Afrika litaendelea kupigania haki zake.

Marais wengine waliozungumza katika maadhimisho hayo na kuwapongeza wakenya katika miaka 50 ya Uhuru wao ni pamoja na Joyce Banda wa Malawi, Ali Bongo Ondimba wa Gabon na Goodluck Jonathan.

Kenya inaadhimisha miaka 50 ya uhuru ikiwa imepiga hatua kubwa ya kuwa na uchumi imara miongoni mwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali.

Kenya ilipata uhuru wake tarehe 12 Desemba,1963, kutoka kwa Muingereza baada ya harakati za mapambano ya kundi la Mau Mau zilizoanza katika miaka ya 1950.

Mau Mau lilikuwa ni kundi la wapiganaji wazalendo lililopambana na viongozi wa kikoloni na walowezi wa Kizungu kwa ushirikiano na Hayati Jomo Kenyatta ambaye baada ya uhuru alikuwa ni Rais wa kwanza kuliongoza taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.