Pata taarifa kuu
UKRAINE

Kiongozi wa Upinzani nchini Ukraine aitisha maandamano zaidi

Kiongozi wa Upinzani nchini Ukrain Arseniy Yatsenyuk ametoa wito kwa waandamanaji kujitokeza kuandamana zaidi mjini kiev wakiwa na matazamaio ya kufanikiwa kuuondoa utawala wa raisi Viktor Yanukovych baada ya kikosi cha kutuliza ghasia kuingilia kuwasambaratisha waandamanaji hao. 

Kiongozi wa upinzani nchini Ukraine Arseniy Yatsenyuk
Kiongozi wa upinzani nchini Ukraine Arseniy Yatsenyuk www.lithuaniatribune.com
Matangazo ya kibiashara

Yatsenyuk amewaambia waandamanaji katika viwanja vya mjini kiev kuwa kamwe hawatasamehe wala kukata tamaa kwakuwa mamilioni yatajitokeza kupinga utawala hadi ujiondoe mamlakani.

Hata hivyo Umoja wa Ulaya EU unafanya jitihada za kujadiliana na mamlaka ya Ukrain ili kuzuia matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji baada ya polisi wa kutuliza ghasia kuwakabili waandamanaji hao katika jiji la kiev.

Katika upande mwingine EU imesisitiza kuwa inataka kuendelezwa kwa uchunguzi wa ghasia zinazoendelea ili kubaini vitendo vya ukiukwaji wa binadamu vilivyofanyika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.