Pata taarifa kuu
SOMALIA

Baada ya kuangukiwa na kura ya kutokuwa na imani naye,Waziri mkuu wa Somalia awatuhumu wabunge kutompa nafasi ya kujitetea

Waziri mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon amesikitishwa na hatua ya wabunge wa Somalia kupiga kura ya kutokuwa na imani naye na kuwatuhumu wabunge kwa kutompa nafasi ya kujitetea.

Waziri mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon,ambaye matokeo ya kura ya kutokuwa na imani naye yamemvua wadhifa wake
Waziri mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon,ambaye matokeo ya kura ya kutokuwa na imani naye yamemvua wadhifa wake RFI
Matangazo ya kibiashara

Abdi Farah Shirdon, ambaye amekuwa waziri mkuu wa Somalia kwa zaidi ya mwaka amejikuta akipoteza nafasi yake baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye baada ya kukataa shinikizo la kujiuzulu kutoka kwa raisi wa taifa hilo Hassan Sheikh Mohamud.

Spika wa bunge la somalia Mohamed Osman Jawari, alibainisha kura 184 kati ya 249 za wabunge waliopiga kura walipiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Aidha Spika Jawari ameongeza kuwa waziri mkuu huyo na serikali yake ataendelea na majukumu yake hadi atakapoteuliwa waziri mkuu mwingine.

Wabunge wa Somalia walipiga kura ya kukosa imani na Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon, kwa tuhuma za ufisadi na kusabisha mgogoro ndani ya serikali aliyoiunda mwaka mmoja uliopita.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.