Pata taarifa kuu
ISRAEL-ROMA

Waziri mkuu wa Israel Netanyahu na Papa Francis wazungumza juu ya Iran

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekutana na kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis leo jumatatu katika sehemu ya ziara yake Roma ambapo ameonesha msimamo wake dhidi ya Mpango wa Nyuklia wa Iran.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis azungumza na Waziri mkuu wa Israel
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis azungumza na Waziri mkuu wa Israel news24
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza waziri Netanyahu alipokelewa na mwenyeji wake Papa ambaye anataraji kufanya ziara yake mashariki ya kati mwakani.

Papa Francis na zairi Netanyahu walikutana kwa takribani dakika 25 na kufanya mazungumzo ya siri.

Waziri mkuu wa Israeli Netanyahu alimtafsiria papa Francis kitabu cha baba yake Benzion Netanyahu kiitwacho The Origins of the Inquisition in Fifteenth Century Spain" ambacho alikitoa maalum kwa kiongozi huyo ambaye amemfananisha na mchungaji mkuu wa urithi.

Aidha waziri Netanyahu na papa Francis wametarajiwa kufanya mazungumzo yanayohusu pande mbili ya Israel na Palestina ambayo yaliendelea mwezi Julai baada ya miaka mitatu ya kukwama.

Chanzo kimoja kutoka Israel kimeeleza kuwa ziara ya Papa Francisi huko Mashariki ya kati huenda itafanyika kabla ya raisi wa Israel Shimon Peres kumaliza awamu yake ya uongozi mwezi Julai ingawa hakuna tarehe rasmi iliyotajwa.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.