Pata taarifa kuu
DRC

Makundi mengine ya uasi nchini DRCongo yakubali kuweka silaha chini ili kurejesha amani Mashariki mwa nchi hiyo

Makundi ya uasi katika eneo la mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, yamekubali kuweka silaha chini na kurejeshwa katika maisha ya kiraia kwa baadhi na wengine kujiunga na jeshi la serikali la FARDC. Hapo jana viongozi zaidi ya kumi wa makundi ya uasi wamekutana kwa mazungumzo na gavana wa Mkoa wa Kivu ya kaskazini Julien Paluku kwa upande mmoja na kwa upande mwingine na waziri wa kitaifa wa mambo ya ndani Richard Muyej Mangez anayezuru katika eneo hilo kuzungumzia kuhusu hatua hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mmoja miongoni mwa viongozi wa makundi hayo ya waasi Izabayo Kabasha Ephrem kutoka kundi la MPA Nyatura amesema waliingia maguguni ili kukabiliana na waasi wa kundi la M23, lakini kwa sasa kundi hilo sio kitisho tena, hakuna sababu zozote za kuendeleza mapigano.

Upande wake waziri wa kitaifa wa mambo ya ndani Richard Muyej baada ya kuwapokea viongozi hao, amewaahidi kuwa serikali italitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo suala hilo.

Kundi la waasi la M23 lilisambaratishwa hivi karibuni baada ya kuzidiwa nguvu na majeshi ya serikali FARDC yanayoungwa mkono na vikosi vya Umoja wa Mataifa.

Licha ya kusambaratishwa kwa kundi hilo, bado muafaka baina ya serikali ya Kinshasa na kundi hilo bado haujafikiwa, juma lililopita pande hizo mbili zilishindwa kuafikiana mjini Kampala ili kutia saini mkataba wa amani utakaomaliza mzozo wa eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.

Wito umeendelea kutolewa kwa makundi ya wapiganaji kujisalimisha na kuweka silaha chini bila shuruti kabla ya kuanz akwa oparesheni ya kuyatokomeza makundi mengine huko Mashariki mwa DCRongo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.