Pata taarifa kuu
URUSI

Uchunguzi waanza kubaini chanzo cha ajali ya ndege iliyosababisha vifo vya watu 50 Urusi

Serikali ya Urusi inaendesha uchunguzi kubaini sababu za chanzo cha ajali ya ndege iliyosababisha vifo vya watu 50, kitengo cha dharura nchini humo kimearifu kuwa ndege hiyo aina ya Boeing 737 iliwaka moto baada ya kuanguka wakati ilipojaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Volga mjini Kazan ikitokea katika uwanja wa ndege wa Domodedovo mjini Moscow.

(©Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa kamati ya uchunguzi ya usafiri katika mkoa wa Volga, Alexander Poltinin amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kusema iliwaka wakati ilipojaribu kutua kwa mara ya pili, Alexander anesema uchunguzi huo utaangalia utajaribu kutafuta sababu za ndege hiyo ilishindwa kutua kwa mara ya kwanza.

Inahofiwa kuwa huenda hali mbaya ya hewa ni chanzo cha ajali hiyo kwani kulikuwa na mvua wakati ajali hiyo ilipotokea jumapili usiku.

Kituo cha televisheni cha serikali ya Urusi kimeripoti kuwa ndege hiyo ilitua kilometa 500 toka uwanja wa ndege wa Kazan na kisha kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Picha za video toka katika uwanja huo zimewaonyesha vikosi vya uokoaji vikijaribu kuzima moto katika eneo ambalo ndege hiyo iliwaka moto.

Miongoni mwa raia wa kigeni waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni pamoja na raia wa Uingereza Donna Carolina Bull na raia mmoja wa Ukraine, Margarita Oshurkova. Wengine waliopoteza maisha wanasadikiwa kuwa ni raia wa Urusi.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Tatarstan imefanya kazi kwa miaka 23 toka ilipoanza kutoa huduma mwaka 1990.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.